AJALI MBAYA IMETOKEA MPAKANI MWA TANZANIA NA BURUNDI

NA, ANKO G

Ajali mbaya imetokea mpakani mwa Tanzania na Burundi (Kabanga-Kobero) ambapo ajali hiyo imehusisha gari la mizigo (Lori) kugonga magari madogo leo Februari20, 2025.

Aidha madhara ambayo yametokana na ajali hiyo simamia.com bado inasubilia ripoti ya Mamlaka husika.

Vilevile ikumbukwe kuwa eneo hilo limekua likisababisha ajali marakwamara kutokana na mtelemko mkali uliopo katika eneo hilo pamoja na kutokuwa na mistari inayo onyesha kubadilisha njia kutokana na kuwa ni eneo la mpaka ambapo anaeyetokea Tanzania anatakiwa kubadilisha mkono (left hand) na kuhamia mkono wa kulia (Right hand) na anaye toka Burundi kuhama kutoka mkono wa kulia (Right hand) na kuhamia mkono wa kushito (Left hand).

Hivyo basi kuna haja ya serikali zote mbili kufanya maboresho katika eneo hilo ili kupunguza ajali zinazojitokeza mara kwa mara zinazo pelekea athari kwa binadamu na vyombo vya moto.

Pia miongoni mwa maboresho katika eneo hilo ni pamoja na kupanua eneo la barabara na kuboresha njia za kubadilisha mkono kutokana na nchi hizi mbili kuendeshea vyombo vya moto kwa kutumia mikono tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *