Nzaza: Soko La Kimataifia Sio Simulizi Tena, Zaidi Ya Bilioni Zadondoshwa Kata ya Kabanga

Billion 1 na million 200 Zatengwa kumalizia ujenzi wa soko KABANGA.

Siku ya Tarehe 6 December 2024 kumeahuhudiwa ukabidhiaanaji wa Kuanza ujenzi wa soko la kimkakati nzaza.

Soko Hilo linatarajiwa Kuanza ujenzi wake tarehe 20 December 2024 na Kumalizika Tarehe 25 May 2025.

Mbunge wa Jimbo la NGARA Mh Ndaisaba George Ruhoro ameshuhudia makabidhiano ya utiaji Saini ujenzi wa soko la kimkakati la kimataifa Nzaza,ambapo katika tukio Hilo Mbunge amesema Kwa miaka 10 iliyopita soko lilikuwa limesimama kujengwa lakini yeye amefanikisha jambo la ujenzi wa soko kuendelezwa.

Mbunge amesema Juhudi za Rais Samia, Mbunge Ruhoro na Diwani Hafidh wa kata ya Kabanga katika kufanikisha Umaliziaji wa ujenzi wa soko Hilo.

Mpaka Sasa mkandarasi amelipwa PESA ya awali million 181 kama pesa ya awali Ili aanze ujenzi, Mbunge amemuomba mkandarasi kazi ya vibarua awape watu wa kabanga na sio wengine.

Lingine Mbunge amewaasa wananchi wa kabanga kuwa walinzi wa vifaa na pale wanapomuona mtu anataka kuiba basi kufikisha taarifa Kwa viongozi wa ulinzi na usalma.

Ndaisaba amesema ifikapo mwakani katika kipindi Cha uchaguzi wananchi wa Ngara wamchague Rais Samia maana ameleta Maendeleo kabanga na Ngara kiujumla.

Posted in Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *