MTOTO WA DARASA LA IV ANAHITAJI MSAADA

Habari za majukumu viongozi! Kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa siku ya jumamosi tarehe 17/5/2025 mwanafunzi Kelvin John wa drs la IV S/M Nyabisindu akiwa anatokea shule alidondokea banzi akicheza na wenzake. Utumbo ulichanika kitendo kilichopelekea Murgwanza hospitali waukate na kuunga upya baada ya kutoa kipande kilichoharibika.

Changamoto kubwa iko kwenye gharama za matibabu kwani anaishi na mama baada ya wazazi wake kutengana. Kijana anaishi na babu na mama aliolewa kwa mume mwingine huko Murgwanza. Mama uchumi wake ni mdogo sana kuhimili gharama hizo. Hadi jana jioni gharama ilikuwa zimefikia sh 160,000/=.

Yeyote mwenye kuguswa na hali ya mtoto huyu tunaomba asaidie kuchangia matibabu kupitia namba hii ya mwalimu mkuu Gabriel Elibariki Mollel 0765941925 maana tunakoelekea shule itatupiwa mzigo huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *