Na Mwafrika:
Simamia.com ilipata nafasi ya kuzungumza na Mh Diwani Hafidh wa kata ya Kabanga kuhusu mambo mbalimbali ndani ya kata na Halmashauri,ambapo katika kata anayoiongoza amesema tangu aingie Madarakani ametimiza mambo takribani yote.
Kwanza Kwa upande wa Barabara anasema alipoingia alikaa vikao na wenyeviti wa vijiji na vitongoji Kwa lengo kuwaomba waonyeshe maeneo ambayo barabara zitaboreshwa ama kuanzisha mpya,na aliwaomba kutumia pesa za mfuko wa kuhudumia watu wenye mahitaji(Tasaff)kutumia fedha hizo kuboresha barabara.

Pia Kwa Upande wa Elimu amesema alipoingia tu Madarakani mwaka 2020 alifanikiwa kuwaunganisha walimu ambao WALIKUWA hawapatani yaani kuweka umoja,pia tangu aingie Madarakani Shule mbalimbali zimepata Madarasa mengi mfano Kabanga Sekondari imepata vyumba 15 vya Madarasa,mabweni 2 pamoja na vitu na meza.
Pia Kwa upande wa Afya amefanikiwa kuomba Kituo Cha Afyaambalo mpaka Sasa kwa Nguvu ya wananchi na michango kutoka Kwa jamii mbalimbali wanakaribia Kuanza ujenzi huku wakisubiria Pesa kutoka Serikali Ili kumaliza ujenzi huo wa kituo cha Afya kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Murukukumbo.
Vilevile Kwa upande wa Utawala Bora Diwani Hafidh amefanikiwa kusikiliza kero za wananchi wa kata Kwa kutembelea vitongo vyote 25 katika Kata ya Kabanga na kutatua kero na zingine kuzitafutia ufumbuzi.
Hivyo Bado kabanga changamoto zipo IKIWEPO ukosekanaji wa uhakika wa maji kutokana na Mradi wa Serikali uliogharimu zaidi ya Milioni 900 za Kitanzania KUKOSA Nguvu yameme wa kutosha kusukuma maji hayo na haya yamesemwa na Hafidh ambapo mradi huo umepatikana katika kipindi Cha Utawala wake.
Lakini pia Hafidh akizungumzia kuhusu wananchi wanavyompenda hasa kutoka katika kata za jirani amesema yeye anaona ni kwasababu kwanza anapenda kuunganisha watu,pili yeye sio muogoa kwenye kuusema ukweli na kutetea maslahi ya wananchi hasa Katika kata ya Kabanga.
Hata hivyo amezungumzia kuhusu wageni kama wataaminiwa basi wanaweza hata KUGOMBEA na kuwaongoza wananchi katika Jimbo la NGARA na pia amesema anauogopa sana Ubungeila wananchi wakiamua basi Kila mmoja anaweza kuongoza Ili mradi anagombea awe na Sifa sahihi.

