HEMA LA NZAZA LIKO HOI KWAKUKOSA MATUNZO

NA,MWANDISHI WETU.

Ni miezi kadhaa tangu liwekwe hema katika soko la kimkakati lilipo Nzaza katika Kijiji cha Kabanga kata ya Kabanga iliyopo Wilayani Ngara Mkoani Kagera kwaaji ya kuboresha mazingira ya wafanya biashara wa matunda kama vile Parachichi na Ndizi.

Muonekano wa hema kwasasa

Hata hivyo simamia.com imeshuhudia hema hilo likiwa limechanika huku nguzo za hema hilo zikionesha dalili za kudodoka.

Vilevile hema hilo limegeuka kuwa eneo la watoto kuchezea michezo mbalimbali kama inavyo onekana kwenye picha.

Watoto wakicheza chini ya hema la Nzaza

Pia simamia.com imefanya mahojiano na mtu mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Imani huku akigoma kuchukuliwa picha ambaye amesema kuwa hema hilo limekosa matunzo sawsawa na makusudio ya hema hilo kuwekwa katika enoe hilo na badala yake ameshauri ni vyema hema hilo lihamishwe na kuwekwa katika soko moja wapo katika masoko yaliyopo katika kata ya Kabanga ili kusaidia wafanya biashara ndogondogo kupata kivuli wakati wanapofanya biashara zao.

Muonekano wa hema la Nzaza kwasasa

Imani amemalizia kwa kusema kuwa viongozi wasimamie mali za uma vizuri kwasababu wanaposhindwa kufanya hivyo wanarudisha maendeleo nyuma na kuiingizia hasara serikali na kodi za wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *