Bukoba ilikusanyika kumuaga mwanaharakati, mtoto wa Bukoba, na zawadi tunu kwa mkoa wa Kagera. Mamia ya watu kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni wamekusanyika Bukoba kumpumzisha mpendwa wa wengi, Justin Kimodoi aliyepatwa na umauti huko Texas nchini Marekani.
Zifatazo ni picha mbali mbali za wale waliobahatika kuungana katika kumuaga na kutoa heshima zao za mwisho Justin Kimodoi. Kwa wale ambao hawakubahatika kufika Bukoba walitumia mitandao mbali mbali ya internet katika kumuaga huyu kinara aliyependa watu na ambaye katika uhai wake aligusa watu mbali mbali.



















































