KAGAIGAI AMESHIRIKI MISA TAKATIFU YA USHEMASI PAROKIA YA RWINYANA JIMBO KATOLIKI RULENGE NGARA

Mamia ya watu wamehudhulia misa takatifu ya kuwapandiasha Daraja Mafrateri wanne kuwa Mashemasi Misa ambayo imeongozwa na Askofu Severine Niwemugizi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara Misa hiyo imefanya Parokia ya Rwinyana kata ya Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera.

Aidha Misa hiyo imehudhuriwa na watu kutoka nje wa wilaya ya Ngara pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na taasisi akiwemo aliyekuwa Katibu wa Bunge na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye kwasasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la utangazaji (TBC) na Mwenyekiti wa kamati uchangiaji wa kanisa kuu Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara (Cathedral) Kitaifa Stephen Kagaigai ambapo uchangiaji utafanyika February 23, 2025 na mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Doto Mashaka Biteko akimwakilisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Hivyo basi Askofu Niwemugizi ametumia Misa hiyo kuwatangazia waumini kushiriki tukio hilo la uchangiaji litakalo fanyika Jijini Dar es salaam.

Vilevile Kagaigai amepata nafasi ya kumzungumza na baadhi ya watu baada ya Misa na kuweza kubadilishana nao mawazo.

Pia Kagaigai amepata nafasi ya kula chakula cha Pamoja na Mapadri pamoja na waumini huku akipata nafasi ya Kuzungumza na Askofu Severine Niwemugizi wakati wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *