KAGAIGAI MGENI RASMI UZINDUZI WA WIMBO WA DUNIA IFURAHI KWAYA YA MT VICENT WA PAULO

NA,ANKO G

Aliyekua Katibu wa Bunge na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye kwasasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la utangazaji (TBC) Stephen Kagaigai amealikwa kuwa mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa wimbo Dunia ifurahi kwaya ya Mt Vicent wa Paulo Kigango cha Ngundusi Kabanga Ngara leo Desemba 15, 2024.

Aidha moja ya changamoto ambayo imewasilishwa na kwaya hiyo ni kukosa akiba kwenye mfuko ambapo Kagaigai amechangia kiasi cha Tsh Milinioni Moja (1,000,000) kwaajili ya kuwezesha mfuko huo kuwa na akiba itakayo weza kusaidia mambo mbalimbali ya kwaya.

Vilevile Kagaigai amechangisha wadau mbalimbali walio hudhuria hafla hiyo kiasi kisicho pungua Tsh Milioni Moja na Laki Nne kwaajili ya kurekodi Albam ya kwaya hiyo itakayo kuwa na nyimbo Nne huku kila wimbo ukigharimu Milioni Mbili.

Pia Kagaigai amechangia Fedha kiasi cha Tsh Milioni Nne (4,000,000) kwaajili ya kuwezesha maandalizi ya Albam hiyo huku mke wake kichangia mchango wa kushona Sale za wanakwaya wa kwaya hiyo.

Kagaigai amemalizia kwa kuwataka waumini wa kanisa la Roman Catholic Kigango cha Ngundusi-Kabanga Kuiendeleza amani iliyopo na kama akitokea mtu atakayejitokeza kuvuruga amani hiyo atakua adui wa kanisa na adui wa taifa la Tanzania na kuliahidi kanisa hilo kuendelea kushirikiana nalo katika mambo mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *