Madhara ya Mvua Kali Huko Bukoba

FAMILIA 18 ZAKUKOSA MAKAZI BUKOBA KUTOKANA MVUA KUBWA ILIYONYESHA APRIL 30 MWAKA HUU ILIYOAMBATANA NA UPEPO MKALI HUKU MIGOMBA 4198 IKIATHIRIWA.

Na johansen Buberwa – Kagera

Zaidi ya Kaya 54 kwenye vitongoji vitano ndani ya vijiji viwili tarafa ya Bugabo Halmashari ya Bukoba Mkoani Kagera nyumba zao zimeathiriwa na Mvua Kubwa iliyoambatana na upepo Mkali uliodumu kwa muda wa saa moja na nakupeleke familia 18 kukosa makazi huku migomba 4198 kuharibika.

Akizungumza na Dar 24 Media Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima hii leo mei 03,2025 amesema Kamati ya Usalama ya wilaya hiyo ileweza kwanda kwenye vijiji hivyo mei 02 mwaka huu na kujionea kwa namna ya athari ilivyoweza kuvikumba vijiji hivyo na tayari Serikali ipo kwenye mchakato wa kuratibu vitongoji vyote namna wa namna ya kuwasaidia wanachia hao ambao wamepata madhara ya kuharibikiwa mali zao. 

“Kwa sasa familia zile amabazo zimeathiriwa na makazi wanakijiji wenzao tunaomba wanaendelea kuwasaidia  wananchi waliothiriwa na mvua za upepo katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kulifanyia ufumbuzi jambo hilo na wananchi tuendelee kujenga nyumba ambazo ni imara”amesem Sima.

Awali akisoma taarifa ya athari zilozovikumba vijiji hivyo mtendaji wa Kata ya Kishanje Mpandabilima Esk amesema Kijiji Kishanje vitongoji vilivyoweza kuathiriwa vitongoji viwili ambavyo ni Mwijambele Bugashani na Kijiji Bumai viliathiriwa vitongoji vitatu ni Buhinda Kanyamayenje pamoja na Kandago na nyumba 19 n miti 41.

“Na uharibifu mwingine wa mazao ni Magimbi Mihogo na Vanila ilikuwa tarehe 30 mwezi April mwaka 2025 majira ya saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa tatu na nusu asubuhi”amesema Mpandabilima.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Bukoba Vijijini Jesca Ndamukama amesema wanatoa pole kwa wanchi hao ambao wamepata athari za mvua hizo ndani kipindi hiki amabcho ni kigumu kwa upande wao na kuwaomba waendelee kuwa na subira wakati jambo hilo likiwa linashughulikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *