MAMIA YA WATU WAJITOKEZA KWENYE MAZISHI YA KIMODOI

NA,ANKO G

Mamia ya watu wamejitokeza kwenye shughuli ya mazishi ya Justine James Kimodoi ambayo yamefanyika leo April 22,2025 nyumbani kwao Bukoba mkoani Kagera.

Picha ya Marehemu Justine James Kimodoi

Aidha Kimodoi alifariki wiki kadhaa zilizo pita akiwa Texas Marekani ambapo mwili wake uliwasili jumapili ya pasaka nyumbani kwao Kagera.

Hata hivyo Kimodoi amekua kivutio cha wana Kagera katika enzi za uhai wake kwa kuhamasisha maendeleo ya Kagera kwa kuanzisha miradi kama Parm trees Project kwaajili ya kulinda mazingira na kupendezesha mji wa Bukoba, Ijuka Omuka Festival,Kagera women Festival 2024,Kushiriki Buhaya Festival n.k

Pia kipindi cha uhai wake amekua akiwasaidia watu kupata fursa mbalimbali na kuhamasisha miradi ya maendeleo huku kiu yake alitamani Kagera iliyo safi kimazingira na Kagera ya watu wenye umoja.

Ikumbukwe kuwa Kimodoi amezaliwa mwaka 1973 na kufariki mwaka 2025 akiwa katika harakati zake za utafutaji nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *