NA,ANKO G
Baada ya sintofahamu kwa wananchi wa kata ya Kabanga iliyopo Wilayani Ngara Mkoani Kagera juu ya ujenzi wa soko la kimkakati la Nzaza huku wengine wakidai ujenzi huo umesimamishwa simamia.com imefika katika eneo la Nzaza kwa lengo la kujiridhisha kama ujenzi huo umesimamishwa.

Aidha simamia.com imeshuhudia shughuli za ujenzi wa soko hilo zikiwa zinaendelea mapema leo Februari12,2025.
Ifahamike kuwa soko hilo ni soko la kimkakati linalo tarajiwa kumhudumia mataifa yanayo iunda afrika ya Mashariki.

Vilevile soko hilo linatarajiwa kuanza kutumika mwezi Juni 2025 kama ilivyo tangazwa mwishoni mwa mwezi Desemba 2024 katika siku ya utiaji saini kwa mkandarasi aliye kabidhiwa mradi huo shughuli iliyoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro mbele ya mkutano wa wananchi wa kata ya Kabanga.
Matumaini ya wakazi wa Wialaya ya Ngara ni kuona soko hilo likianza kutumika mwezi Juni ili kuondokana na historia ya soko hilo.