Waliotia Nia Ubunge, Jimbo La Ngara

Ni vizuri kujua waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge, Jimbo La Ngara. Hadi Makala hii inaandaliwa, daftari la waliochukua fomu kama ishara ya kutaka kuwakilisha Wilaya ya Ngara linaonyesha kuwa wana Ngara 14 wamejipima na kuona wanafaa kutumikia watu wa Ngara kama Mbunge.

Kutokana na taratibu za chama chao, wajumbe watatathimini sifa za hawa wagombea kumi na nne na kuwachuja ili wabakie na tatu bora tuu. Majina ya hizi tatu bora ndizo zitakazorudishwa na kuingia kwenye mchuano mkali tena mpaka mshindi atakapopatikana. Na hapo Jina moja litalopatikana ndilo litapewa hadhi ya kugombea kiti cha Ubunge na wapinzani wengine kwenye uchaguzi mkuu.

Mpaka majina matatu yatapotangazwa, haijulikani Wilaya ya Ngara itamuajiri yupi kati ya hivi vinala 14 vilivyojitathimini na kujiona vinafaa kuiwakilisha Ngara kule Bungeni, Dodoma.

Timu nzima ya Simamia Media Group inawatakia mchuano mwema na kushukuru kila mgombea wa viti mbali mbali kwa kujitoweni kuitafuta Ngara Njema. Uzinzi wa Ngara ni jukumu la kila Mwana Ngara na hili jukumu linaweza kutimizwa kwa njia mbali mbali, ikiwemo kushiriki kikamilifu katika zoezi zima la uchaguzi, iwe ni kwa kuwania nafasi fulani, kupiga kura ama kusindikiza zoezi zima la kupiga kura ili likamilike kwa ushindani wa kweli na kwa salama kamili.

1. Lameck Jaston

2. Herbert Muhile

3. Eliud Ruzige

4. Dotto Bahemu

5. Ndugu Ndaisaba George Ruhoro (Ananatetea kiti kwa maa nyingine)

6. Restuta Binambi

7. Hilal Ruhundwa

8. Vumilia Gwanori

9. Shimi Gahanga Station

11. Josias Charles

13. Steven Kagaigai

14. Philemon Sengati

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *