Serikali imewataka wamiliki wa viwanda vya ndani kuhakikisha wanatengeneza mabomba ya maji kwa kuzingatia ubora na viwango vya kimataifa vitakavyokidhi soko la ndani  ili kuleta tija katika ujenzi wa miradi ya maji hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu waziri wa maji Mhandisi Marryprisca Mahundi baada ya kutembelea na kukagua shughuli za uzalishaji wa mabomba katika kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji kinachomilikiwa na kampuni ya kahama oil mills kilichopo wilayani kahama.
Alisema kuwa wizara ya maji inaendelea kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa na kiwanda hicho katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini na kuwataka wamiliki wa kiwanda hicho kuhakikisha wanazingatia ubora wake ili kuleta tija katika miradi maji hapa nchini.
âTunatekeleza miradi mbalimbali ya maji hapa nchi KOM ni wadau wetu,sisi kama wizara tunaomba mzalishe mabomba imara ambayo hayatapasuka pindi tutakapo yatumia,lengo letu ni kuwaunga mkono wawekezaji wazawa kwenye shughuli wanazozitekeleza,âalisema Mahundi.
Kwa upande wake Mkurugeni wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kahama (KUWASA) mhandisi Allen Marwa alisema kuwa kwa sasa wanatumia wanatumia mabomba hayo kutoka katika kiwanda hicho kutokana na ubora wake na yanapatikana kwa bei nzuri ikilinganishwa mabomba kutoka nje ya nchi.
Nae meneja wa kiwanda hicho Bryson Edwad alisema kuwa kwa sasa soko la mabomba limeongezeka maradufu baada ya serikali kuanza kununua mabomba ya maji katika kiwanda hicho na kumwahidi kuwa wataendelea kuzingatia ubora na maelekezo yote ya kitaalamu ili kuhakikisha wanaongeza ushindani katika soko la afrika mashariki.
Awali akitoa taarifa ya ukezaji kwa Naibu waziri wa Maji Mahundi, ya wilaya ya kahama, Anamringi Macha mkuu wa wilaya hiyo, alisema bado wanaendelea kutoa maeneo bure kwaajili ya shughuli za uwekezaji wa viwanda mbalimbali na kuwaomba watanzania kujitokeza ili waweze kuwekeza katika eneo hilo.
Recent Comments