Wakazi wa Jimbo la Muhambwe Kibondo Mkoani Kigoma, wametakiwa kufanya maamuzi ya Busara katika uchaguzi wa Mbunge unaotarajiwa kufanyika may 16 mwaka huu, kwa kumpigia kura Kiongozi anaefaa kuwatumikia kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili
Akiongea kwenye Mkutano wa hadhala uliofanyika Mjini Kibondo kwa lengo la uzinduzi wa Kampeni za chama cha mapinduzi, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Ccm ambaye pia ni waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Jimbo la Muhambwe linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji hivyo ni vema wananchi wakamchagua Mtu anayeweza kuwasaidia
Akimuombea kura Mgombea kupitia chama hicho Frolens Samis Majaliwa amemtaka mgombea huyo kuondo mashaka kwa kuwa chama chake kinatambua uwajibikaji wake uliotukuka na kuwataka Wanamuhambwe muchagua mgombea huyo
ââSerikali inafaham na inatambua changamoto zinazolikabili Jimbo hili na iliziweze kutatuliwa ni lazi apatikane kiongozi mahili atakayeweza kushirikiana na wananchi na serikali kwa ujumla hivyo naomba mumchague Dr Frolence Samizi kwakuwa anaweza kupambana
Nao baadhi ya Makada wa chama hicho Katibu wa Itikadi na uenezi Ccm Shaka Amdu Shana na Christina Mdeme Naibu Katibu Mkuu Ccm Bara  wakiendelea kumuombea kura mgombea wa Ccm wamewataka wananchi hao kuwa na msimamo wa kwa kusikiliza sera za wagombea na kuwapima huku yeye mwenyewe akiwataka wanamuhambwe kumuamini na kuahidi kutowaangusha iwapo kama atapewa nafasi kuongoza jimbo hiloKwa upande wao baadhi ya wananchi ambao ni Lazaro Shami na Geradina wamesema Paschal kulingana na changamoto zinazo wakabili ndani ya jimbo la muhambwe wanahitaji kiongozi amabaye anajitambua na na anatakayekuwa akisikiliza maoni yao na kero kabla ya kwenda Bungeni kwa kuwa jimbo hilo lina matatizo mengi ikiwa ni Pamoja na ukosefu wa masoko ya bidhaa za mashambani na miundombinu ya elimu na afya
Uchaguzi huo unafabyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Atashasta Nditiye aliyefariki Februari 12 mwaka hu una uchaguzi huo utafanyika may 16 mwaka huu
Recent Comments