KATIKA kuondoa upungufu wa vitabu kwa wanafunzi nchini Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imekabidhi jumla ya vitabu 173,990 kwa ajili ya shule za Msingi na vitabu 2,714 kwa ajili ya shule za Sekondari, Wilayani Muleba, mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya vitabu hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila, amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa upungufu wa vitabu kwa wanafunzi.
Aliwaagiza Wakurugenzi wa Wilaya, Maafisa Elimu na Walimu wote kuhakikisha vitabu vinatumika kama ilivyokusudiwa.
“Tunataka Wilaya ya Muleba iwe kinara wa elimu kwa maana ya ufaulu, kuongoza kitaifa na inawezekana kwa sababu tayari Rais Samia Suluhu Hassan, ametupa vitabu kupitia TET.
“Naamini vitabu hivi vitatumika kama vilivyokusudiwa,” ameeleza.
Kwa upande wake, Afisa Elimu wa shule za Msingi, Mwalimu Severine Musyangi, amesema vitabu hivyo vitasaidia kupunguza uhaba wa vitabu uliokuwepo.
Amesema vitabu hivyo vitawezesha kufikiwa kwa wastani wa mwanafunzi mmoja, kitabu kimoja.
Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession.
He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.
Recent Comments