Kiukweli siku hizi kwenye mapenzi, mahusiano au ndoa kumekuwa na migogoro mingi na kutengana kila kukicha ambapo jinsia zote hukumbana na suala la kuachika ila leo tutaangazia zaidi upande wa wanawake, ambapo wengi wamekuwa wakiachika au kujikuta wakishare mabwana. Sababu Zinazopelekea Wanawake Kuachika au Kushare Mabwana
i) Uvivu, wanawake wengi wa sasa ni wavivu kwenye suala zima la kitandani na mahaba, eti wanadai wamechoka na mihangaiko akirudi nyumbani yeye anakula tu halafu analala, hapo ujue ndio hawezi amka mpaka asubuhi anapokwenda kazini.
ii) Hawajitumi wakiwa kitandani yaani atakavyo kaa ndio hivyo hivyo mpaka mwisho wa mchezo, haangaiki wala hajihangaishi hajaribu vitu vipya wala mitindo mbalimbali.
iii) Mwanamke akipata kazi husumbua kabisa anakuwa busy na kujifanya amechoka kama mwanaume hajachoka kumbe wote wametoka kazini.
iv) Kama mume hana mood yaani hajisikii yeye pia naye mood hukata yaani hajisikii, kiufupi hawezi kumleta mumewe kwenye mood ya mapenzi hajisumbui kufanya utundu kwani nae anajiona yuko juu hana huo muda.
v) Siku zote husubilia yeye aanzwe , yeye kumuanza mumewe hataki . Yaani mpaka uanze kumchezea na kumuimbisha kama vile demu mpya kumbe ndiyo mkeo.
vi) Akipata pesa yeye hizo ni za kwake na matumizi yake tu binafsi, majukumu kwenye familia yeye hataki keshajitoa, pesa za mwanaume ndio zitumike hadi kumnunulia pedi zake.
vii) Wanawake wana maneno mengi hadi muda mwengine huwakosea heshima waume zao, mwanamke kuongea ni kawaida lakini ikizidi huwa ni kero kwa mwanaume na kupelekea kupoteza maelewano.
viii) Wanajali marafiki zako kuliko hata waume zao wa ndani yan atawajali marafiki zako ili kulinda na kuficha makucha yake kuliko hata mume aliye muoa ambapo hii ni mbaya maana huweza hata kulala na moja ya marafiki wa mume ambapo hii ni aibu kubwa.
ix) Matumizi ya mitandao huwaponza sana wanawake wa sasa, ambapo kwa sasa wengi hufatilia zaidi umbea na kujipost ambapo hii hupelekea ndoa kuvunjika mara kwa mara.
Recent Comments