Recent Comments

DC SAME MHE. KASILDA MGENI AKUTANA NA KAMATI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIANI.

By Mussa Mathias Mar 17, 2024

DC SAME MHE. KASILDA MGENI AKUTANA NA KAMATI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIANI.

Na. Musa Mathias. 

Email. Mussamathias573@gmail.com

Serikali imeitaka Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Misitu Duniani pamoja na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii, ufanisi na uadilifu mkubwa.

Hayo yameelezwa na  Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni wakati wa mazungumzo  na wanakamati wa maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Misitu na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa ambayo Kitaifa yatakayofanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kuanzia Machi 18, hadi Machi 21, 2024 ambayo ni siku ya kilele.

‘Ni wajibu wa kila mwanakamati kufanya kazi kwa kasi, ari na kwa nidhamu huku akisisitiza kuwa kazi hiyo ya kuadhimisha Siku ya Misitu na Upandaji Miti Kitaifa ina maslahi mapana kwa Taifa’. Amesema DC wa Same.

Aidha, ameipongeza Kamati hiyo kwa namna ambavyo wameandaa siku hiyo adhimu ikiwa na matukio mbalimbali ikiwemo maonesho ya bidhaa ya misitu na nyuki, warsha na tukio la Mgeni Rasmi kupanda mti wa ukumbusho.

Pia amesisitiza umoja na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya maandalizi ya maadhimisho hayo miongoni mwa wanakamati hao ili kuleta mafanikio.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Idara ya Misitu na Nyuki Bw. Daniel Pancras ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri ambayo imeifanya na kuisisitiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Misitu kutoka Idara hiyo, Bw. Seleboni Mushi ameahidi kuwa wao kama kamati wataendelea kushirikiana kuhakikisha maadhimisho hayo yanafana na kufanyika kwa weledi mkubwa.

Mwisho.