Ni,Vuta ni Kuvute. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na wingi wa wagombea nafasi mbali mbali za Uongozi hasa Udiwani na Ubunge katika kata na Majimbo ya uchaguzi ambayo yanaweka historia hapa Nchini.
Hali hiyo, inaibua maswali yasiyo na majibu kutoka kwa wananchi,kwakuwa katika chaguzi mbali mbali zilizowahi kutokea hakukuwahi kuonekana pia idadi kubwa ya wakigombea kama inavyoonekana kwa sasa.
Jimbo la Msalala pekee lina wagombea 44. Jimbo hili linapatikana katika wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga,ambalo kwa mihula mitatu limekuwa likiongozwa na Bw.Ezekiel Maige aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili wakati wa Uongozi wa awamu ya nne.
Tofauti na Chaguzi zilizopita, Mwaka huu Maige ana upinzani mkali kutoka ndani ya Chama chake. Jumla ya wagombea 43, nayeye akiwemo wanakuwa 44 ambao wamechukua na kurudisha fomu sasa wanajinadi mbele ya wapiga kura ili kuomba kupewa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwapitisha kugombea Ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba Mwaka huu.
Jimbo la Msalala ni miongoni mwa majimbo matatu ya wilaya ya Kahama ambayo ni Kahama Mji,Msalala na Ushetu. Uchaguzi kama huu unafanyika pia Kahama mji,ukiwahusisha vigogo wawili wa kisiasa Mbunge anayemaliza muda wake Jumanne Kishimba,na mbunge wa zamani James Lembeli.
www.simamia.com itaendelea kukufahamisha kuhusu Uchaguzi huu.
Tunakaribisha matangazo,wasiliana nasi kwa simu 0756432748 na Whats app +255756432748
Recent Comments