KAHAMA
Jumla ya Wanachama 99 wa Chama cha Mapinduzi CCM wamejitokeza kugombea nafasi za Ubunge katika Majimbo ya Msalala,Ushetu na Kahama Mjini ikiwa ni siku ya pili Tangu kuanza zoezi la utoaji  fomu za kuwania nafasi Udiwani na Ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu huku vijana wakionekana kuhamasika kwa wingi ikilinganishwa na uchaguzi uliopita
Akizungumza na vyombo vya  baada ya kukamilisha siku ya pili ya utoaji wa fomu za ubunge na Udiwani Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Bw.Emmanuel Lameck Mbamange amesema asilimia kubwa ya wagombea ni vijana, na kwamba kati ya wagombea wote wanawake 9 wamejitokeza kuwania nafasi za ubunge katika majimbo hayo
Amesema kuwa katika Jimbo la Kahama Mjini mpaka sasa wamejitokeza wagombea 53 kati yao wanawake ni sita ambapo nusu ya waliochukua fomu ni vijana ikilinganishwa na uchaguzi uliopita jambo ambalo linaonesha kukua kwa Demokrasia ndani ya CCM
Aidha, Bw. Mbamange amesema mpaka sasa Jumla ya wagombea 18 wamejaza na kurudisha na kuwataka wagombea kutojihusisha na vitendo vya kampeni kabla ya muda jambo ambalo linaweza kusababisha kukosa sifa na kuondolewa katika nafasi.
âKatika Jimbo la Msalala mpaka sasa kunawagombea 33 ambapo mwanamke ni mmoja huku Jimbo la Ushetu likiwa na wagombea 13 huku mwanamke akiwa ni mmoja ,natarajia mapaka tarehe ya mwisho wagombea wengi watajitokeza kuomba nafasi mbalimbali za Ubungea na udiwani ili waweze kuwatumikia wananchi katika maeneo yao,âalisema Mbamange.
âLengo letu sio kuwakosesha pindi mnapojaza fomu zenu hakikisheni mnajaza kwa ufasaha na hata kama ikitokea umekosea kujaza usianze kunungâunika njoo ufisini tutakupatia fomu zingine ili ujaze kwa ufasaha na hii ndio demokrasia  inayotakiwa ndani ya CCM mpya,âalisema Mbamange.
Katika hatua nyingine Mbamange amewataka wagombea kutojihusisha na vitendo vya kampeni kabla ya muda jambo ambalo linaweza kusababisha wakakosa sifa na kuondolewa katika nafasi wanazoziomba na badala yake wazingatie maelekezo yaliyotolewa na chama katika utekelezaji wa zoezi hilo.
âMsianze kujipitisha pitisha kwa wananchi kwa kutoa rushwa mamlaka zinazosimamia sheria zipo macho muda wote ukishachukua fomu jaza rudisha na kisha subiria maelekezo ya chama ili uwe salama hatupendi kusikia mgombea Fulani kakamatwa kwa kuhushishwa na vitendo vya rushwa,âalisema Mbamange.  Mwisho
www.simamia.com na Simamia TV tunakaribisha Matangazo ya Biashara,habari na Matukio. Aidha wagombea wote mnakaribishwa kujinadi na kuzungumza na wapiga kura.
0756432748
Recent Comments