Serikali wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga imepiga marufuku wapiga debe wanaofanya shughuli zao katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama kwaajili ya kurejesha ustaarabu na kupunguza kero kwa wasafiri
Tangazo la marufuku limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Anamringi Macha wakati akizungumza na wasafiri,wamiliki wa mabasi na wahudumu wa Stendi
Mkuu huyo wa wilaya amesema wapiga debe licha ya huduma zao wamekuwa kero kwa wasafiri kutokana na utaratibu wa kugombania abiria ndani na nje ya kituo kikuu cha mabasi hivyo Serikali haiwezi kuwavumilia
Hata hivyo, Bw.Macha ametoa agizo kwa jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi na usalama katika kituo cha mabasi na kuwataka kuchukua hatua wapigadebe wote watakaoneana kukaidi agizo hilo
Wakizungumzia tamko la serikali, baadhi ya wapiga debe Noel Arusha na Remi Kibada wameiambia www.simamia.com kuwa, amri ya mkuu wa wilaya itatatekelezwa lakini italeta athari kwa baadhi ya wapiga debe waliokuwa wakitegemea kazi hiyo pekee kuendesha maisha yao
Aidha, kutokana na amri hiyo Mwenyekiti wa Stendi kuu ya mabasi mjini Kahama Salum Said amesema agizo la Mkuu wa wilaya litatekelezwa na kwamba atakayekiuka masharti atachukuliwa hatua licha ya kueleza kuwa vurugu za wapigadebe zinachochewa na baadhi ya wamiliki wa mabasi kushindana kibiashara.       Mwisho
Recent Comments