Wauzaji na wamiliki wa dawa mhimu za Bianadamu wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za afya ili kuepusha madhara kwa wananchi
Wito huo umetolewa na Bi. Winifrida Moremi, mfamasia kutoka Baraza la famasi Tanzania Idara ya elimu na Mafunzo wakati akitoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya wamiliki wa maduka ya dawa katika Chuo cha Sayansi za afya Kahama
Bi.Moremi amesema ni wajibu wa kila mhudumu na mmiliki wa duka la dawa muhimu za bianadamu kuzingatia sheria na kanuni ili kuhakikisha huduma zao zinaboresha afya za wananchi
Awali katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu 74, mkuu wa chuo cha Sayansi za afya Kahama Dkt.Mashaka Cosmass ameataka wahitimu kutumia elimu waliyopata kutoa huduma
Bw.Jovitho Jovin, na Neema Christopher ambao ni baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo muhimu yaliyoanza tangu March mwaka huu wanayataja kuwa nguzo muhimu katika huduma zao kwa jamii.
Recent Comments