CHANGAMOTO YA NGARA KATIKA KUPATA MBUNGE MWENYE UCHUNGU NA MAENDELEO YA NGARA NA WANA NGARA
Ana andika Josias Charles
Nimeamua leo kuandika Ujumbe huu ambao ninaamini utaweza kuwafungua macho baadhi ya watu kuhusu ni wapi haswa tunakwama katika kufikia malengo yetu ya kuwa na wawakilishi wenye uwezo wa kushirikiana na Wananchi, wataalamu na wadau mbalimbali katika kuleta maendeleo ya Jimbo la Ngara. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo kwà kiasi kikubwa zimekuwa zikiturudisha nyuma kwà vipindi vya miaka mitano mitano:-
1. RUSHWA
Hii ndiyo sababu kubwa mno ya Ngara kupata Viongozi katika nafasi za kuchaguliwa (Ubunge na Udiwani) wasio na sifa lakini pia wasiothamini kabisa Maendeleo ya wana Ngara. Viongozi wanaoingia madarakani kwà Rushwa wamekuwa hawawasikilizi Wananchi, hawawshirikishi Wananchi kuhusu Masuala ya Maendeleo na hata hawathamini mchango wa wasomi na wataalamu mbalimbali katika kuleta maendeleo ya Ngara. Watu hawa wanaamini kuwa wana uwezo wa kutenga fungu la Fedha na kuligawa kwà Wananchi masikini na wajumbe wa Vyama vyao ili wateuliwe kugombea Ubunge. Viongozi wa namna hii hujaa dharau na majivuno dhidi ya masikini kwà kiasi kikubwa mno.
2: Ukanda
Hii ni Hoja ambayo wengi hawaizungumzii lakini binafsi nitaizungumzia maana mficha uchi hazai. Kwenye suala hili tumekuwa na kasumba ya watu ambao wanaamini kuwa kijiti cha uongozi Ngara kinapaswa kuwa mpokezano kati ya Bushubi na Bugufi, wengine wamekuwa wakienda mbele zaidi wakitaka Ukanda fulani u dominate kuongoza Jimbo la Ngara. Na hata wengine wameenda mbele zaidi wanatamani Ngara igawanywe yawe majimbo mawili ili kila Ukanda ujiongoze. Kutokana na Hoja hii watu wanaoendekeza Ukanda Hawaii tayari kumpa support mtu wa Ukanda mwingine hata Kama ana uwe mkubwa kabisa jatika kuleta maendeleo ya Ngara. Mambo haya yametufanya Ngara kuendelea kupata Viongozi wabovu pia kupitia upenyo huu. Binafsi suala hili huwa linanitoa sana machozi. Kwa wageni kwenye siasa ya Ngara haya mambo hawawez kuyaelewa watahisi ni hadithi za abunwasi. Ndugu zangu wana Ngara huu mtizamo hauna Tija kwetu. Tuwapime watu kwà vizio vya uwezo wao wa Uongozi na sio kigezo butu Kama hiki
3. Ubinafsi
Hili nalo ni tatizo lingine kubwa. Kuna baadhi ya watu ambao wao hugombea Ubunge Ngara kwasababu tu ya ubinafsi wa kutaka kutimiza malengo yao binafsi (kuinua uchumi wa Familia, kutafuta namna ya kulinda biashara kwà kutengeneza makampun na kutumia nafasi yako kuhakikisha kila Tender inafanyika kupitia makampun yako na marafiki zako). Watu hawa kwao Jambo la Muhimu sio Maendeleo ya Ngara, wao wako tayari kupambana kwà gharama yoyote washinde uchaguzi hata Kama kuna mtu ana uwezo wa Uongozi zaidi yao ilimradi tu walinde maslahi yao na Kundi lao. Huu ni ubinafsi na dhuruma ya hali ya Juu sana kwà Wananchi kwani kila baada ya uchaguzi tukipata kiongozi wa hovyo basi Ngara inaumia kwà miaka mitano.
4. Vijana kutumika Kisiasa kubeba agenda za wagombea wenye fedha
Kuna mchezo umekuwa ukifanywa na baadhi ya wagombea kwà miaka mingi ambapo huwa wanatengeneza watia nia fake ambao hawa kazi yao ni kuongeza Idadi na kazi yao ni kupambana na mgombea mwenye nguvu huku wakimlinda mgombea mwenye fedha aliyewapandikiza. Mfano, Kama mgombea Ubunge mwenye fedha elimu yake ni ndogo sana basi hupandikiza mgombea anayekuja kupiga kampeni kwà kusisitiza kuwa Elimu Haina maana kabisa jatika suala la Uongozi Kama Ubunge na Udiwani. Mgombea huyu pandikizi hupambana kwà kila njia kugawa kura za mgombea mwenye sifa ya kielimu kwa manufaa ya aliyempandikiza. Kama mgombea sio muajiriwa na makazi yake yako Ngara basi hupandikiza mtia nia ambaye kazi yake ni kupambana na wagombea wazaliwa wa Ngara ambao wanaishi nje ya Ngara kutokana na majukumu yao ya kazi mfano kuna watu wameajiriwa na Taasisi za Kimataifa, Taasisi kubwa za Serikali , vyuo vikuu nk ambao kwà namna moja ama nyingine lazima wafanye kazi nje ya Ngara. Haoa ndipo wagombea dhaifu kupitia Kwà watia nia fake huibuka na Hoja “Tunataka mgombea tunayekula, kunywa na kulala naye kila siku” Kwà wageni wa Siasa hawawezi kuhusu huu mchezo lakini huu ni moja ya mambo ambayo yameifanya Ngara yenye Border karibia nne kuwa moja ya Wilaya ambazo hazijachangamka kiuchumi mpaka Sasa.
4 WASTAAFU KUTAFUTA FURSA NA VIJANA KUTAFUTA AJIRA
Kuna watu ambao wamekuwa kwenye Utumishi wa Umma kwa kipindi kirefu lakin kwà muda wote hawajafanikiwa kujipanga kimaisha. Wastaafu hawa huwekeza nguvu kubwa ya Fedha kutafuta Ubunge kwà ajiri ya manufaa yao na familia zao badala ya kuwatumikia Wananchi, lakini pia kuna Kundi la Vijana ambao hawana ajira nao hauamini kwa kugombea watapata fursa ya kuweza kufikia malengo yao binafsi na sio malengo ya wana Ngara. Kwenye Chaguzi mbalimbali zilizopita na hata hizi za sasa nimepata nafasi ya kuingoea na baadhi ya Vijana, wengi wanatia nia kwà lengo la kukuza CV ili waonekane na mamlaka za uteuzi nk. Huu mtizamo kiukweli sio wa kizalendo hata kidogo maana Ngara inahitaji kupata watu ambao kweli kutoka ndani ya mioyo yao wana dhamira ya dhati kabisa kuwatumikia Wananchi.
5. SUALA LA TAJIRI NA MASIKINI
Hii pia ni changamoto kubwa kwà Ngara katika kupata kiongozi mzuri wa kuwakilisha Wananchi wa Jimbo la Ngara. Kumekuwa na kasumba ya wenye pesa kutengeneza Syndicate ya wenye fedha kuwa support matajiri wenzao kwenye siasa ya Ngara kupambana na masikini. Kuna baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wako tayari kutoa Lita 2000 za Mafuta kum support Tajiri fulani kufanya kampeni, Kuna watu wako tayari kuwajazia Petrol Bodaboda wa mji mzima kwà gharama zao kwa kuwa wana maslahi na Mgombea fulani ambaye ni Tajiri. Kuna watu wako tayari kutoa milion 10 kuongeza nguvu kwà Tajiri tena kwà mikataba. Manufaa yote haya masikini wa Jimbo la Ngara hata mama ana uwezo mkubwa katika Uongozi kwà namna Gani hana namna ya kuyapata. Kwa maana hiyo mtu masikini hapati fursa ya kuongoza Jimbo la Ngara sio kwasababu hana uwezo wa kuongoza bali kwasababu hana uwezo wa kifedha.
Wananchi wenzangu wa Ngara tunayo kila sababu ya kujipima kwà dhati kuhusu dhamira zetu katika kuchukua Form, tunayo kila sababu ya kuwapima wale tunao wasupport kuhusu uwezo wao wa Uongozi, tunayo kila sababu ya kuamua kusimamia ukweli na sio ujirani, urafiki, undugu, kwà manufaa yetu binafsi. Ngara ni muhimu kuliko Jambo lolote , tunapopoteza Jimbo kwà kumpatia mtu dhaifa basi hasara ya miaka mitano ni yetu sote.
Kwà leo naishia hapa mpaka wakati mwingine.
Wako katika Ujenzi wa Ngara
Josias Charles
Hii Simamia inasema eti: Simamia is your best source for news, entertainment, music, blah blah blah wakati hakuna new yoyote hapa tangu 2015. Ukisoma Simamia unaweza kufikiri rais bado ni Kikwete. Tangu ianzishwe 2015 adi leo 2020 haijaweka habari zaidi ya 15. Tatizo hakuna stuff Simamia. Ni jeshi la mtu mmoja. Hakuna journalists ana copy habari kutokakwenye vyombo vingine vya habari vya kuaminika. Pia anaweka habari anazo sikia social media.