Recent Comments

KATIBU WA BAWACHA SINGIDA ATEMA CHECHE

By Simamia Journal Jul 7, 2020

KUELEKEA UCHAGUZI WA OCTOBER 2020 NAPENDA KUWASHAURI NDG ZANGU WA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Twende pamoja na mimi BEATRICE ASKEY KATIBU BAWACHA MKOA WA SINGIDA.

Kumekuwa na desturi ya baadhi ya wanaccm kuzani kuwa vyama vya upinzani havina haki kwenye Taifa hili wamekuwa wakizani ni wao pekee wenye haki ya kuwa huru na Taifa hili.chuki dhidi ya upinzani imekuwa kubwa sana kana kwamba mpinzani ni adui wa Taifa na kusahau adui wa Taifa ni maradhi,ujinga na umaskini.

Tunapojiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa October 2020 nchi yetu imetajwa kuwa nchi ya uchumu wa kati ushauri wangu sasa wanaccm wajikite kuwaeleza watanzania namna ya uchumi wa kati ulivopatikana kwa njia gani ili waweze kueleweka kwa jamii kama ambavyo sisi tutakavyoenda kuelezea kero za watanza ambazo kwa muda mrefu zimeshindwa kutatuliwa kwa vitendo hasa jamii ya wakulima na wafugaji,maji kero ya maji na utoaji wa huduma za afya usiyo wa uhakika.ukosefu wa ajira na elimu bure ilivotekelezwa kwa kiwango cha chini mno kiujumla tujikite kwenye hoja za kutatua matatizo ya watu.

Chama cha mapinduzi kina serkali inayojinasibu imetekeleza sijui hofu yao ipo wapi imekuwa na hofu na wapinzani hususa chadema wakionekana tu wanamagari na bendera za chama wanafuatilia mpaka mwisho kama kiongozi wa chama anafanya kikao tena cha ndani lazima apate shida ikiwezekana kuzuiliwa ama kukamatwa kabisa.hofu hiyo ni ya nini wakati serkali imetekeleza?

MWISHO

Tunapoingia kwenye uchaguzi tuingie na hoja sio chuki zisizo na faida kwa Taifa.sisi CHADEMA tumejiandaa kama kawaida yetu kuwaeleza ukweli watanzani wakitupa ridhaa nini tutawafanyia tukiwa madarakani.

ASANTENI SANA

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv