Recent Comments

KUNA NGUVU KUBWA KATIKA UKIMYA

By Simamia Journal Jul 8, 2020

Kalamu ya miambili ya Mwl.Jonathan Kwizera

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini wanafunzi wanaokaa kimya darasani asilimia kubwa hufaulu mitihani yao vizuri?

Ulishajiuliza kwa nini watu wengi wenye mafanikio makubwa huongea kidogo Sana na huchukua muda mrefu wakiwa kimya kwenye mambo yanayo wahusu?

Ulishawahi kuulizwa swali ukatoa jibu la ndio lakini baada ya dakika kadhaa ukatamani kutengua kauli useme hapana?

Ulishajiuliza kwa nini maranyingi unajutia maamuzi yako?

Inawezekana hujachochea nguvu ya ukimya

Unapokaa kimya unaruhusu akili yako kupima madhara au faida ya maamuzi yako.

Unapokaa kimya unafuta mzunguko zunguko wa kelele nyingine kwenye akili yako na unakua na uwezo wa kuamua Kama wewe.

Ukikaa kimya unaruhusu mwendelezo wa jambo uliloanzisha awali kwa sababu unaruhusu akili kukumbuka kwa nini ulilianzisha Suala hilo.

Ukikaa kimya tena ukafumba macho kidogo unaruhusu kiwango cha juu cha kumbukumbu.

Watu wengi wakikumbwa na changamoto wanaanza kutafta vitu vya kufanya ili wasahau yaliyotokea , watabonyeza simu au computer, watajibizana na watu eti wanatoa ya moyoni lakini nguvu ya ukimya ni imara kuliko zote.

Watu wengi wasio na nguvu ya ukimya wanaingia Sana kwenye uhasama na watu wengine, wanasahau dhamira ya mambo yao, wanafanya mambo mengi kwa wakati mmoja , wanapata wasiwasi na maamuzi yao badae, wanakumbwa na mawazo , hupoteza ubunifu na huingia hasara ya vitu vingi katika maisha .

Jifunze kuruhusu nguvu ya ukimya itawale kabla ya Maamuzi makubwa Katika maisha yako.

The Top is For You

Mwl.Jonathan Kwizera
Author & Motivational speaker
#NdotoYanguAcademy
ndotoyanguacademy@gmail.com
+255627177566

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv

One thought on “KUNA NGUVU KUBWA KATIKA UKIMYA”

Comments are closed.