Na, Juventus Juvenary-Ngara.
Ni wakati wa maamuzi. Maamuzi yanayotakiwa sasa ni yale yenye kutoa dira na mwelekeo kimaendeleo kwa miaka 5 ijayo itakayoleta mabadiliko katika sekta mbalimbali na faraja kwa wananchi kupitia wawakilishi watakaopatikana kwenye  Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu
Ni uchaguzi utakaowezesha upatikanaji wa Madiwani,Wabunge na Rais. Wawakilishi watapatikana kupitia Uchaguzi ambao tayari mchakato wake umeanza, ambapo mpaka sasa watia-nia wameanza kujitangaza na kuainisha vipaumbele vyao huku zoezi la Uchukuaji fomu likitegemea kuanza 14-17 julai mwaka huu
www.simamia.com leo imeweka kambi katika jimbo la Ngara Mkoani Kagera. Imezungumza na mmoja wa wawatia nia kwa nafasi ya Ubunge,kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi
Ainaitwa Ndaisaba George Ruhoro, mkazi na mzaliwa wa Kijiji cha Katerere Kata ya Kanazi wilaya ya Ngara ambaye tayari ametangaza nia ya kuugombea nafasi ya Ubunge kwa lengo la kushirikiana na wananchi wa Ngara kuleta mabadiliko kimaendeleo
Katika mahojiano na www.simamia.com Bw. Ndaisaba anaitaja dhamira na malengo yake ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ngara ambayo kwa mkiaka 5 iliyomalizika lilikuwa likiongozwa na Ndugu Alex Raphael Gashaza kuwa ni kutaka kushirikiana vema na wananchi wa jimbo hilo ,uongozi wa wilaya pamoja na Serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa vitendo,utiifu,Uadirifu, na ufanisi unaoendana na mahitaji ya serikali inayoongozwa na Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Anasema maamuzi yake ya kutangaza nia kugombea Ubunge pia yanakolezwa na nia yake ya kutaka kutumia ujuzi,maarifa na taaluma aliyonayo kwenye utafutaji wa rasilimali watu na fedha, kujenga mahusiano yenye tija na kushawishi mipango ya maendeleo ili kufanikisha maendeleo ya uhakika katika sekta ya maji,Afya,Elimu ,Nishati ya umeme kwenye vitongoji na maeneo ambayo hayajafikiwa,miundombinu ya barabara pamoja na miundominu ya mawasiliano ya simu ambako mtandao unasumbua
Aidha, Bw. Ndaisaba anasema kuwa anawiwa kugombea ili ashiriki kuwezesha kuvuatia uwekezaji kwenye kilimo na viwanda vidogovidogo,madini ya Nickel na manganese ambapo anaamini kwakufanya hivyo atasaidia kuzalisha ajira kwa vijana na watu wengine wenye nguvu ya kufanya kazi na kuchochea kuhuwisha mzunguko wa fedha hivyo kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja ,wilaya na Taifa kwa ujumla
Anaongeza kuwa, ameamua kugombea Ubunge wa jimbo la Ngara ili kufuatilia,kushawishi na kutengeneza mazingira wezeshi ya kukamilika kwa maandalizi na kuanza kwa ujenzi wa Barabara za Rulenge-Keza-Nyakahura na nyingine zinazohitaji ukarabati na matengenezo ili kurahisisha usafirishaji wa vitu na watu  ili kuchochea Uchumi na kuboresha maisha ya wananchi
Bw. Ndaisaba George Ruhoro ambaye kitaaluma ni mwanasheria anasema nia yake ya kugombea ni kumaliza kiu ya wana Ngara kutosikika Nchini hasa Bungeni na kwamba akichaguliwa ataitangaza Ngara na kuifanya isikike na kutambulika vema.
Sisi, www.simamia.com na Simamia TV, tunamtakia kila la kheri na mafanikio mema Ndugu Ndaisaba George Ruhoro na watia nia wengine wenye mapenzi mema na majimbo yao.
Kwa watia nia na wagombea wote,mnakaribishwa kuleta matangazo yenu,nasi tutawasogeza karibu na wananchi. Pakua App ya Simamia TV kupitia Play store, install kwenye simu yako kwaajili ya kupata Habari na matukio wakati wowote.
Wasiliana nasi kwa simu +255756432748/WhatsApp +255756432748.
Recent Comments