MFAHAMU LAMECK KUMBUKA JASTON ,MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NGARA ALIYEAMINIWA KATIKA UMRI MDOGO KUWA MSHAURI WA AFRIKA KATIKA MASUALA YA AJIRA NA BIASHARA,NA MSHAURI WA UMOJA WA MATAIFA KATIKA MASUALA YA BIASHARA ZA KIMATAIFA.
Ni mzaliwa katika kijiji cha Ngundusi Kata ya Kabanga wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
Ni mmoja wa wagombea 43 wanaoomba ridhaa ya Chama cha mapinduzi kugombea Ubunge katika jimbo la Ngara . Wakati wimbi la Kutia nia likichukua kasi ya juu sana, huku watu wakiamini kuwa idadi kubwa ya wagombea katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu imechochewa na maslahi ya kifedha na madararaka , hali ni tofauti kidogo kwa kijana huyu Lameck kumbuka Jaston ,ambaye kwa sasa anaishi mjini Geneva nchini Uswisi.
www.simamia.com imefanya mazungumzo na Lameck Kumbuka Jaston, ambaye anaeleza kuwa aliamua kuacha majukumu na fursa nyingi katika viunga ya Umoja wa Mataifa ilimradi tu ashirikiane na wananchi wenzake wa jimbo la Ngara, kuhakikisha wanakuwa pamoja bega kwa kuiendeleza Ngara
Katika mazungumzo yake na mtandao huu, anadhirisha kuwa fedha,mshara na vyeo alivyotumikia havina umuhimu wowote kama havijabadirisha maisha ya watu wa jimbo la Ngara,jamii iliyomlea na kumkuza
Lameck,alikata ticket yake ya kutokea Geneva kupitia Ufaransa , Ethiopia, Dar es salaam Bukoba na kisha aelekee Ngara kutangaza nia,na kuwaeleza wananchi yaliyo moyoni mwake na ndoto yake juu ya Ngara.
Aidha ajali ya gari aloyoipata siku mbili kabla ya safari ilipelekea kuvurugika kwa ratiba ya kufika mapema, ambapo Miongoni mwa watu kutoka kampuni ya kusaidia kupeleka gari katika matengenezo alibainika kuwa ana virusi vya Korona hivyo yeye akawa mmoja wapo wa tu waliowekwa Karatini hadi tarehe 21, huku kura za maoni zikipigwa jumatatu ya tarehe 20.
Licha ya mkwamo wa Safari yake,hakukubali kabisa ndoto yake kwa wanangara ipotee. Lameck Kumbuka Jaston anakishukuru Chama Cha Mapinduzi kikwa kuweka utaratibu mzuri unaompa haki mwanachama yeyote mwe sifa kuchukuliwa fomu fursa ambayo ilimuwezesha kuchukua fomu,kuzija na kuzirudisha kwa muda muafaka.
Lameck Kumbuka Jaston ni msomi wa shahada tofauti za uzamili (Masters) katika maswala ya Sheria za kimataifa na Diplomasia, Lameck kwa sasa anafanya utafiti wa shahada ya Uzamivu (PhD) katika siasa ya uchumi (Political Economy)
Kama msomi na mtu aliyeshika nyadhifa kubwa kimataifa, anaweka wazi sera zake kuisogeza mbele Ngara kimaendeleo,na kueleza vitu anavyotamani kufanya kwaajili ya maendeleo ya Ngara na wanachi wote kuwa ni pamoja na kuwawezesha Wanangara kujiletea maendeleo wenyewe kwa kutumia semina na elimu ya ujasiriamali, kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii kuzalisha mazao ya kutosha huku yeye akitafuta wanunuzi, na kutumia mtandao na uzoefu wake kutafuta masoko ya bidhaa za kilimokwa bei inayomnufaisha mkulima. Aidha amesema pamoja na mikakati mingi aliyonayo ni Kuongea na makampuni ya zana za kilimo,vifaa vya ujenzi ujenzi na wadau muhimu popote pale Duniani ili kufanikisha mambo makuu 7 ya kwanza ambayo anayataja kuwa ni:-
- Afya
- Elimu
- Maji
- Makazi bora
- Barabara
- Umeme  na   7.Ajira hasa katika kilimo na ufugaji
Waswahili wanasema, nyota njema huonekana asubuhi. Â Ukiwauliza watu wa Ngundusi, kijijini alikozaliwa Lameck, wanamuelezea kama kijana ambaye pamoja na kuishi ulaya mawazo yake na moyo wake unaishi nyumbani kwao!. Amekuwa msitari wa mbele kusaidia watu wasiojiweza, kuchangia maendeleo ya jamii ambapo kama sehemu ya mchango wake amefanikisha kujenga chumba cha Darasa katika shule ya msingi aliyosomea
www.simamia.com ilipomuuliza Lameck kama hawezi kuwaletea maendeleo wanangara akiwa huko huko Uswisi amejibu kuwa yeye haamini katika Pesa na kichango ya kutumwa kwani hii ni sehemu ndogo ya mkakati wa kuleta maendeleo. Anaamini kukaa na watu,kuongoza kwa mfano,kufanya kazi pamoja na kuwahamasisha akiwa kama mfano wao katika maisha yake ya kila siku.
Sisi www.simamia.com tunamtakia kila lakheri katika Mchakato wa Uchaguzi.
kwa habari na matangazo wasiliana nasi kwa simu +255756432748/whats app 255756432748
Recent Comments