Tukio hilo limetokea Julai 17 mwaka huu ambapo mchimbaji mmoja katika kitalu cha Wachimbaji wadogo wa Namba 5 Kata ya Mwakitolyo Wilaya ya Shinyanga ambapo Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joseph Kumburu amesema imetokea majira ya saa 6 mchana wakati wachimbaji zaidi ya watano walikuwa wakitoka ndani ya Duara baada ya kumaliza kazi kwenye duara namba  56D.
Mhandisi Joseph Kumburu amemtaja marehemu kuwa ni Michael T. Salumu mwenye umri wa miaka , Mkazi wa Kijiji cha Masungura, Wilaya ya Meatu na kwamba alikuwa akichimba madini ya dhahabu kwenye duara hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 20
Aidha, Afisa Madini huyo ameeleza kuwa Sababu za kifo cha mchimbaji huyo zimetokana na marehemu kuanguka ndani ya duara baada kukosa nguvu na kupasuka kichwa na kueleza kuwa kutokana na matukio ya vifo yanayojitokeza mara kwa mara ,katika machimbo ya Mwakitolyoyamefungwa kwa siku tatu ili kupisha ukaguzi maalum wa maduara yaliopo katika leseni 23 za Wachimbaji wadogo.
Kusitishwa kwa uchimbaji huo, kutafanyika kwa awamu kuanzia leseni za eneo la Namba 5 na kufuatia leseni nyingine za Na4 hadi 1,na kuwataka Wachimbaji wadogo kuhakikisha wanazingatia Sheria za uchimbaji na maelekezo wanayopewa na Wataalam wa Madini na Jeshi la Polisi.
Katika kuhakikisha usalama na ulinzi wa maeneo hayo, Afisa Madini huyo ameambatana na  Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Madini, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkurugenzi kusimamia zoezi la ukaguzi na kushauri hatua za haraka za kuchukua kwa maduara yote yatakayobainika kuwa ni hatari kwa afya, Usalama na utunzaji wa mazingira.
Sambamba na hilo, Afisa Madini amewataka Wachimbaji hao kuhakikisha wanazingatia Sheria za Madini na maelekezo wanayopewa na wakaguzi kwa kufukia mashimo yote ambayo yameachwa wazi ili kuepusha madhara na maafa yanayoweza kujitokeza.    Mwisho
Recent Comments