SERIKALI imetangaza rasmi Filamu za Bongo zitakazokidhi vigezo vya maadili na soko, zitaanza kuonyeshwa kwenye Kumbi za Sinema nchini, ili kuwezesha upatikanaji wa soko la kudumu na lenye tija kwa wadau wa tasnia hiyo.
Akizungumza jijijini Dar es Salaam leo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amesema filamu zitakazopata nafasi ya kuonyeshwa kwenye kumbi hizo ni zile zitakazokidhi vigezo vya kimaadili na soko pekee.
âKabla ya kuionyesha filamu kwenye Ukumbi, kwanza itapitia kwenye mchujo mkali wa kupima vigezo vya kimaadili na soko, jambo ambalo litafanywa na kamati maalumu iliyo chini ya Bodi ya Filamu nchini,â amesema.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuwa na soko la kudumu la filamu na lenye tija, pia baada ya kuonyeshwa faida itagawanywa kwa mwenye filamu, mmiliki wa Ukumbi na Serikali.
Amewataka wadau wote wa tasnia hiyo kuongeza ubunifu na ubora wa kazi zao ili zifudhu kuonyeshwa kwenye kumbi hizo.
Kwa mujibu wa Dk. Makyembe, kwa sasa serikali imefanikiwa kubadili kanuni za Sheria ya michezo ya kuigiza ambapo filamu ya kila maudhui itaonyeshwa kwa kuzingatia muda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania Profesa Ezekiel Mutua, amesema mchakato wa kuchuja filamu zitakazokidhi kuonyeshwa kwenye kumbi mbalimbali nchini unaanza rasmi leo.
Amesema kwa hatua ya awali wataanza kuonyesha filamu tatu kwa mwezi.
Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession.
He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.
Recent Comments