Marekani imetoa tahadhari dhidi ya usafiri wa Kenya baada ya idadi ya maambukizi ya corona kuongezeka nchini humo.
Taarifa katika tovuti ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya umesema serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya kukaa nyumbani na kurejesha usafiri na baadhi ya shughuli za kibiashara.
Kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti magonjwa-CDC, inaonekana kuwa kuna kiwango kikubwa cha maambukizi kwa wasafiri na hakuna angalizo la kupunguza tatizo hizo. Wakati huohuo Kenya imetangaza kuwa sekta ya utalii imepoteza mabilioni ya dola katika pato la taifa kuanzia Januari mpaka sasa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Mataifa mengine ya Afrika ambayo yako kwenye kiwango cha hatari ya maambukizi ni pamoja na Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini, Ethiopia, Djibouti, Uganda, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe na nyinginezo.
Aidha watu zaidi ya watu milioni mbili wamepoteza ajira zao katika sekta hiyo nchini Kenya na mamlaka inakadiria kuwa hali inaweza kurudi kama awali mwanzoni mwa mwaka 2023.
Wakati nchi hiyo ikipunguza masharti dhidi ya marufuku ya kutoka nje.Bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Eliud amechaguliwa kuwa balozi wa utalii Kenya wakati taifa hilo likiangalia mianya ya kurejesha utalii wa kimataifa.Article share tools
Recent Comments