Ikiwa bado kikao cha kamati ya maadili na nidhamu cha shirikisho la soka nchini (TFF) kikiwa kinaendelea kusikiliza shauri la utata wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Bernard Morrison mwanamuziki Hamis Mwijuma (Mwana FA) ambaye ni shabiki wa Simba SC amepenyeza taarifa za ndani juu ya kinachoendelea kwenye kikao hicho.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mwana FA amedokeza kuwa, Mahasimu wao Yanga wameshinda shauri hilo na Morrison ni mchezaji wao halali.
âKwa hivo Yanga wameshinda shauri na Morrison ni mchezaji wao halali..kwa hivo kimsingi wana Morrison na Senzo, enhe tunajiteteaje wazee wangu ?â Amendika Mwana FA.
Morrison alitangazwa kujiunga na klabu ya Simba siku chache zilizopita baada ya kuwa na mgogoro wa muda na klabu yake ya Yanga.
Recent Comments