Haji anaeleza kuwa alioga mara ya mwisho zaidi miaka sitini iliyopita
Haji huamini kuwa chakula safi, na kuoga ni hatari kwa maisha ya binadamu
Je umewahi kukaa kwa zaidi ya siku tatu bila kuoga hali ikawa shwari tu? Kwa Amou Haji raia wa Iran, kuoga ni ndoto tu.
Kulingana na ripoti iliyotolewa 2015 haswa baada ya kuhojiwa na jarida la Tehren Times, Haji ndiye amevunja rekodi kuwa mwanadamu chafu zaidi ulimwenguni.
Imebainika kuwa Haji ambaye sasa ana umri wa miaka 85 hajaoga kwa zaidi ya miaka 65. Kulingana naye hana tatizo lolote, kuoga ndiko humpa matatizo..
Haji huamini kuwa kuoga na kula vyakula safi ni njia mojawapo ya kujisababishia magonjwa, kando na hivyo kila anapofikiri kuhusu kuoga, anapatwa na hasira isiyo ya kawaida.
Bwana huyo hunywa zaidi ya lita tano ya maji kila siku, hula vyakula vilivyovunda, mabaki ya wanyama waliokufa na huvuta sigara.
Recent Comments