Familia ya Mbunge wa zamani wa Changamwe Ramadhan Kajembe, imetishia kumshtaki Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe, kwa kutoa matamshi wanayodai yaliidhalilisha familia hiyo, kuhusu maambukizi ya Corona, ambayo huenda yatapelekea unyanyapaa kwenye familia.
Imeelezwa kuwa Mbunge huyo wa Changawe alifariki na kuzikwa nyumbani kwake huku Serikali ikisema kuwa Mbunge huyo wa zamani alifariki kutokana na Virusi vya Corona, wiki chache tu, baada ya mkewe Kajembe kufariki pia kutokana na corona.
Soud Kajembe ni mtoto wa Marehemu Kajembe amesema kuwa kitendo kilichofanywa dhidi ya Baba yao si cha kiungwana na kwamba wamelaani kitendo hicho na kuwataka wale wote waliohusika kusambaza taarifa hizo akiwemo Waziri Kagwe, Waziri wa Elimu pamoja na Gavana Sonko, kuwa maradhi waliyoyapata wazazi wao isiwe sehemu ya kufanyia siasa zao.
Familia hiyo sasa inawapa siku kumi na nne waliohusika kudhalilisha familia hiyo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Waziri wa Elimu George Magohaa, na Gavana wa Nairobi Mike Sonko ambae pia, aliuweka ujumbe wa Kagwe kwenye mtandao wa kijamii, akijikuta kwenye orodha ya kushtakiwa, iwapo hawataiomba familia hiyo msamaha.
Recent Comments