Takriban watu 800 wamekufa kote duniani kutokana kwasababu ya taarifa potofu zinazohusiana na virusi vya corona katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwkaa huu, wanasema watafiti.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Marekani linaloandika taarifa za magonjwa ya maeneo yajito na usafi, unasema kuwa watu wapatao 5,800 walilazwa hospitalini kutokana na taarifa zisizo sahihi juu ya corona zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii.
Wengi walikufa kutokana na kunywa kemikali ya methanol au bidhaa nyingine za kuua viini hatari.
Waliamini kimakosa kwamba bidhaa hizo ni tiba ya virusi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) awali lilisema kuwa “janga la taarifa” zinazozingira Covid-19 husambaa haraka sawa na virusi vyenyewe, huku nadharia potofu, uvumi na unyanyapaa wa kitamaduni vyote kwa pamoja vikichangia vifo na majeraha
Wengi wa wahanga walifuata taarifa zinazofanana na taarifa za kuaminika za kimatibabu-kama vile ulaji wa kiwango kikubwa wa vitunguu saumu au kunywa kiwangi kikubwa cha vitamin mabli mbali kama njia ya kujikinga na maambukizi, anasema muandishi wa utafiti huo.
Matendo haya yote yalikua na “uwezekano wa kusababisha athari mbaya” kwa afya zao, watafiti wanasema.
Utafiti huo unasema kwamba huo ni wajibu wa mashirika ya kimataifa , serikali na mitandao ya kijamii kupambana na “janga la taarifa potofu”,lakini makampuni ya kiteknolojiayamekuwa yakikosolewa kwa kuzorota kujibu taarifa potofu zinapotolewa. Nchini Uingereza sheria za kudhibiti taarifa zenye madhara kwenye mtandao huenda zikawa mbali miaka kadhaa .
Uchunguzi binafsi wa BBC ulibaini kuwa viunganishi(links) za taarifa za matusi, mashambulio ya moto na mauaji kutokana na taarifa potofu juu ya virusi , na kuongea na daktari, wataalamu na wahanga juu ya uzoefu wao.
Tetesi za mtandaoni zilisababisha mashambulio ya watu wengi nchini India na utoaji wa sumu kwa watu wengi nchini Iran. Wahandisi wa mawasiliano wamekua wakitishiwa na kushambuliwa na mitambio ya simu imekuwa ikichomwa moto nchini Uingereza nan chi nyingine kwasababu ya dhana potofu ambazo zilitungwa na kuvumishwa kwenye mtandao .
Mitandao ya kijamii pia husaidia watungaji wa taarifa kutumia janga la virusi vya corona kuuza bidhaa ambazo wanadai zinasaidia kumaliza virusi , na kuwataka wafuasi wao kutoa pesa ili wapewe “madini ya muujiza wa dawa mbadala”, ambayo kiukweli ni blichi iliyotiwa maji.
Huku chanjo zikijitokeza, kuna tisho zaidi ambalo wanaharakati wanaopinga chanjo watatumia jukwaa lililotolewa na mitandao ya kijamii kuwashawishi watu kujikinga. .
Licha ya makampuni ya mitandao ya kijamii kuondoa au kuweka matangazo ya taarifa potofu juu ya chanjo, kura ya maoni ya hivi karibuni nchini Marekani ilionesha kwamba 28% ya Wamarekani wanaamini kuwa Bill Gates anataka kutumia chanjo kuweka kifaa cha kunasa taarifa ndani ya miili yao.
Mafanikio ya ufanisi wa chanjo ya corona yanaweza kukwamishwa kabisa na taarifa potofu , madaktari walikiambia kitengo cha BBC kinachokabiliana na taarifa potofu.
Recent Comments