Mwandishi wa zamani wa BBC Mohamed Moalimu aliponea shambulio la Jumapili dhidi ya hoteli mji mkuu wa Somalia, Mogadishu – kwa mara ya nne amejipata katikati ya mashambulizi ya kundi la al-Shabab katika kipindi cha miaka saba.
Moalimu, ambaye sasa anaongoza Shirikisho la Wanahabari wa Somalia, alimsimulia mwandishi wa BBC Basillioh Mutahi tukio hilo na jinsi rafiki take alivyokuwa miongoni mwa watu 20 waliouawa katika shambulio la Hoteli ya Elite:
Nilikuwa natetemeka. Moyo yangu ulikuwa inanidunda kama dramu huku mwili ukiningishika. Moshi mweusi mkubwa ulikuwa umetanda kila mahali na ilikuwa vigumu kuona vizuri kilichokua kimetokea eneo hilo.
Watu walikuwa wanapiga mayowe. Baadae niliweza kuona uharibifu ulisababishwa na mlipuko huo. Baadhi ya watu waliumizwa na vioo vya madirisha, naw engine walikuwa wanatokwa na damu, huku wengine wakiomba msaada.
Rafiki yangu, Abdirizak Abdi, alitaka kutoroka muda huo. Lakini nilimzuia kufanya hivyo kwa sababu wakati huo makabiliano makali ya risasi yalikuwa yakiendelea lakini alikimbilia upande wa lango la kuingilia.
Nilisubiri hadi nikabainini upande gani milio ya risasi ilitokea, kutokana na mafunzo niliopata juu ya hatua unazotakiwa kuzingatia ukiwa katika mazingira ya hatari.
Nilikuwa naelewa hatua zote, jambo ambalo lilinisaidia, kwasababu niliweza kujionea kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Ndio sababu niliponea.
Nilijua pa kukimbilia, na sikukimbia moja kwa moja bali nilikua nikipiga kona za hapa na pale. Baadae nilikwea ukuta na kuruka upande wa hoteli uliokuwa ukielekea ufukweni.
Makabiliano ya risasi yalikuwa yanaendelea lakini nashukuru niliponea.
Baada ya hapo nilijaribu kumpigia simu rafiki yangu lakini sikufanikiwa kumpata kwasababu simu ilikuwa imezimwa.
Nilijaribu kumtafuta, akiwa hai ama amekufa. Niliona watu wengi baada ya mlipuko wakiwa wamelala chini sajafuni. Baadhi yao walikuwa wanapiga mayowe. Ilikuwa hali ya kusikitisha sana.
Ambulensi zilikuwa zimeanza kufika katika eneo la tukio licha ya kwamba ufuatulianaji wa risasi ulikuwa unaendelea. Kuna mtu aliniambia kuwa Abdirizak amejeruhiwa na kwamba amepelekwa hospitali.
Kwa bahati mbaya, alipigwa risasi na magaidi waliokuwa wakiwamiminia watu risasi kiholela. Alipigwa risasi mguuni na kifuani.
Wakati huo, ilikuwa vigumu kutoka hapo kwasababu polisi walikuwa wamejazana na makabiliano makali ya risasi yalikuwa yanaendelea.
Muda mfupi kabla ya shambulio hilo Abdizirak,ambaye alikuwa akifanya kazi na Wizara ya Habari alinipitia nyumbani kwangu na halo tukatoka pamoja kwa gari kuja hotelini hapo.
Kwasababu magari hayakuruhusiwa kuondolewa katika eneo la tukio nililazimika kukimbia kwa miguu hadi hospitali, lakini nilipofika kwa bahati nilifahamishwa kwamba Abdirizak amefariki.
Ilikuwa siku ya huzuni – na kwa mara ya one nilishuhudia shambulio la kigaidi mjini Mogadishu.
Ilikuwa mara ya kwanza ambayo sikujeruhiwa.
Mwaka 2013 nilikuwa ndani ya majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa wakati wa shambulio la wanamgambo wa al-Shabab- gari langu liliposhambuliwa na bomu kutoka kwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Shambulio lengine ni la 2016, karibu na hoteli ya Lido beach ambapo uso wangu ulijeruhiwa vibaya.
Nililala kwenye damu kwa zaidi ya saa mbili na ilinichukuwa muda mrefu kupona baada ya kupata matibabu katika hospitali za Nairobi na London.
Mwezi Februari mwaka jana katika, shambulio dhidi ya Hoteli ya Maka al Makarama ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa, nilijeruhiwa mwilini na mikononi kutokana na vigae vya kioo.
Lakini nilifanikiwa kutoroka kupitia mpenyo ulioachwa wazi baada ya gari lililokuwa na bomu kulipuka.
Lakini siamini mfanyakazi mwenzangu, rafiki tuliyekuwa pamoja tukinywa kahawa pamoja siku hiyo – amefariki.
Alifariki katika kipindi cha dakika chache. Waelewa ninachosema. Sikupata usingizi kabisa. Nilijaribu lakini nilishindwa. Niliathirika vibaya sana.
Karibu watu 20 walithibitishwa kufa, miongoni mwao washambuliaji wanne na mmoja wa kujitoa muhanga kufa.
Idadi kubwa ya watu – wanaofanya kazi Mogadishu hula wanapendelea kutembelea hotel hilo kupata kikombe cha chai say za mchana.
Nilishangaa sana shambulio hilo lilipotokea kwasababu nilidhani kuwa hali ya usalama imeimarika.
Jamaa zangu wamekuwa wakinishauri nisiende hotelini. Sasa nitafuata ushauri wao kwasababu hiki ni kitu ambacho hakitawahi kuis
Mara hiii familia yangu ilikuwa na hofu kwasababu ilijua Abdirizak amefariki.
Nilipowapigia simu nikiwa hospitali, hawakuamini kwamba niko hai hadi pale waliponiona.
Ilikuwa vigumu kwao kuamini nilivyonusurika – kwa mara ya nne.
Recent Comments