Furaha Dominic, aliyeongoza katika kura za maoni kati ya walioomba nafasi ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kawe Jijini DSM kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amezungumza baada ya chama hicho kumpitisha Askofu Josephat Gwajima aliyeshika nafasi ya tatu katika kura hizo.
âNatoa shukurani zangu kwa wajumbe na nasema nimekubaliana na maamuzi ya chama na nitamuunga mkono huyo aliyependekezwa na chama, Ndugu Askofu Gwajima, lengo letu ni moja tu kama vijana wana CCM ni kukirudisha chama madarakaniâ Furaha
âTunaamini chama kimemchagua mtu sahihi na tunaamini sisi ni asset ya kesho kwa ajili ya chama chetu, na nataka niwaambie wajumbe wote walichukulie hili jambo kwa furaha, ni jambo ambalo limefanyika kwa umakini na wamefanya kwa kufuata vigezo vingi, na naamini chama hakijakoseaâ Furaha
Recent Comments