SERIKALI imetangaza rasmi Vitambulisho vya Taifa, Leseni za Udereva, Hati za kusafiria na namba za simu, kuanza kutumika kusajili wageni wa ndani na nje ya nchi, watakaolala kwenye nyumba zinazotoa huduma za malazi, kupitia mfumo wa kielektroniki wa Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT PORTAL).
Imesema utaratibu huo, utaanza kutumika kwa nyumba za wageni âLodgeâ na Hoteli zilizosajiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kwamba rasmi utaanza kutekelezwa Oktoba mosi, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya usajili wageni wanaolala kwenye Huduma za Malazi kupitia mfumo huo kwa Wamiliki wa Malazi, 200 wa Kanda ya Pwani, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga, alisema hatua hiyo inalenga kupatikana kwa takwimu zitakazosaidia kuboresha sekta ya utalii.
âLengo kuu la kufanya hivi ni kupata taarifa zitakazosaidia Serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kuboresha sekta ya Utalii nchini,â amesema.
Amesema taarifa hizo zitatumika kama nyezo katika kuandaa sera, mikakati na mbinu za kuboresha sekta ya utalii hasa wa ndani ambao mwamko wake umekuwa mdogo kwa wananchi.
Ameongeza kuwa mfumo huo, utatumika katika hoteli, Kambi na âLodgeâ zinazotambulika na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Chitaunga, amewataka wamiliki wote wa nyumba zinazotoa huduma hizo kuhakikisha kuanzia Oktoba mosi, mwaka huu, wanaanza kutekeleza agizo hilo kwani ni takwa la kisheria.
Amewahakikishia wamiliki hao, kuwa taarifa zote za wageni zitatumika kwa ajili ya serikali pekee na zitatunzwa kwa usiri wa hali ya juu.
Samson Nelsa, Â ni miongoni mwa wamiliki wa Huduma za Malazi katika mkoa wa Pwani, amesema mfumo huo ni msaada mkubwa kwa serikali katika kuandaa taarifa za idadi ya watalii.
Amesema pia utawasaidia kuwa na sehemu salama za kuhifadhi taarifa za wateja wao.
Naye Mohamed Juma, mmliki wa Hoteli ya Rainbow, amesema hiyo ni hatua bora na muhimu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na kuongeza kuwa ni vyema kwa wizara kuhakikisha taarifa za wateja wao hazitumiki kwa maslahi binafsi.
Pia ameishauri wizara hiyo, iweke utaratibu imara wa kulinda mfumo huo, ili usishambuliwe na watu wenye maslahi binafsi.
WANANCHI WALONGA
Bakari Msumi, mkazi wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam, amesema mfumo huo utasaidia katika usalama kwa mteja pindi atakapopatwa na changamoto yoyote kwenye nyumba hizo.
Amesema pia utasaidia kudhibiti wahalifu kuingia nchini kwani taarifa zao zitakuwepo kupitia vitambulisho, hivyo hawataweza kufanya lolote kwa hofu ya kukamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Ameongeza kuwa mfumo huo ni msaada katika kuongeza mapato ya serikali, kwani itatambua takwimu za wateja waliopatiwa huduma hizo.
Kadhalika Msumi, ameshauri kuimarishwa kwa usiri wa taarifa za wateja ili zisitumike kwa maslahi binafsi.
Naye Swaleh Ally, mkazi wa Dar es Salaam, amesema ni bora zaidi mfumo huo utumike kwa wageni wanaoingia nchini na kuongeza kuwa kuna hofu ya watoa huduma hizo kukosa wateja kutokana na ugeni wa mfumo huo.
Daaah hii kali mwanangu