VYOMBO vya Habari nchini vimeshauriwa kutojihusisha na wanasiasa wanaohubiri, chuki, kejeli, matusi na kuhamasisha vurugu, kwani kufanya hivyo ni ishara ya kuhatarisha amani ya nchi.
Hayo yalisemwa juzi na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha ADC, Queen Sendiga, alipozungumza na wanahabari jijini Dar es Salam.
Alisema imeshuhudiwa katika majukwaa ya kampeni za vyama vya upinzani zikitumika lugha zisizofaa, jambo ambalo linahatarisha amani ya nchi hivyo, vyombo vya habari visitumike kurusha matangazo ya wagombea wa namna hiyo.
âSisi tukiwa sehemu ya vyama vya upinzani tunasikitishwa na vitendo hivi vinavyofanywa na wenzetu na kwamba hatukubaliani navyo, wanahabari wachuje ipasavyo,â alisema.
Alishauri mamlaka zinazohusika ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa makaini na wanasiasa wanaoonyesha viashiria vyovyote vya kuhatarisha amani wasipewe nafasi.
âKama kuna chama au mgombea anaona hatendewi haki ni vyema afuate utaratibu wa kisheria na kupeleka malalamiko yake kwa mamlaka husika, sio kutumia majukwaa ya kampeni kuhamasisha chuki baina ya watanzania, madhara ya kuvunjika kwa amani ni makubwa,â alisema.
Kwa upande wake mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha AFP, Seif Maalim Seif, alisema muhimu ni wanasiasa kutambua kuwa uchaguzi ni suala la mpito wakati taifa litaendelea kubaki.
Alisema kwa kutambua hilo, kila mwanasiasa atafanya kampeni zake kwa nkudumisha amani, mshikamano na utaifa.
âSisi wote ni wamoja uchaguzi ni mpito, wananchi wanataka kusikiliza sera sio kuwahubiria mambo ambayo yatawaweka kwenye hatari,â alisema.
Naye Cecilia Mmanga, mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokria Makini, alisema kilichofanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kukata matangazo ya moja kwa moja ya wanasiasa waliokuwa wakitumia lugha zisizofaa ndio msingi wa kanuni na sheria unaopaswa kufuatwa na vyombo vyote vya habari.
âVyombo vya habari ni njia ya haraka ya ufikishaji taarifa kwa wananchi kama vitaruhusu wanasiasa wasiopenda amani kuvitumia, tutaipeleka pabaya nchi yetu,â alisema.
Recent Comments