Haya ni mambo matano aliyoyazungumza Mgombea Urais Dr. John Pombe Magufuli (CCM) baada ya kusimama Mlowa ambako Mgombea Ubunge wa CCM ni Livingstone Lusinde, Dr. Magufuli alisimama Mlowa wakati akiwa njiani kuelekea Iringa ambapo haya hapa chini ndiyo aliyoyaongea.
âNileteeni wa CCM ambao ninao uwezo wa kuwatumbua mkinileta mwingne sina uwezo wa kumtumhua pesa zitaliwa na sina cha kumfanya, Mbunge wenu Lusinde ni mchapakazi, narudia Ubunge sio Madegree ni uwezo wa kujenga hojaâ
âNawapenda sana watani zangu Wagogo, naamini kabisa mtanipa kura, tena inawezekana Lusinde akanitafutia Kasichana kazuri ka Kigogo au mnasemaje Wagogo?, si mtanipa?, zege halilali, RC Dodoma mwagize Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma huu mwezi wa tisa ndani ya miezi miwili Barabara ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami ili Wagonjwa wanaougua hapa wawe wanapelekwa Mvumi, tunataka Jimbo hili ambalo lipo karibu na Makao Makuu ya Nchi tulibadilshe liwe lenye kunusanusa makao Makuuâ
Mvumi nina historia nayo nilikuwa na Kaka yangu alikuwa Daktari pale sasa hivi ni Marehemu kwahiyo Mvumi ninaifahamu nilishawahi kumleta Mzee mmoja kutoka Chato ambaye alinishauri Mimi kujiunga na siasa nilimleta pale Mvumi kufanyiwa upasuajiâ
âHata kuhamia Dodoma haikuwa rahisi tumekaa zaidi ya miaka 47 hilo halijawezekana ila sisi tumeweza, tunajenga uwanja wa Ndege mkubwa Msalato, Ndege zote za Kimataifa zitakuwa zinatua hapa, tumejenga Reli ya kisasa, Soko la kissa, Stendi ya kisasa, tunataka kutimiza ndoto ya Baba wa Taifaâ
Recent Comments