Watu wawili wanashikiliwa na vyombo vya dola mkoani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi na mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Iringa Emmanuel Mlelwa aliyeuawa na kutambuliwa siku 6 baada ya kifo chake.
Akizungumza katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa,mkoani Njombe.Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya.amesema watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo huku wakiendelea na upelelzi wa awali.
Aidha amewata wananchi kuwa wavumilivu kwa sasa kwa kuwa vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo
âSasa hivi tupo katika kampeni kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu,lakini kampeni haiwezi ikatumika kuvunja amani.Kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,tutawasaka wahusika kwa nguvu zote kuhakikisha wametiwa mbaroniâalisema Marwa Rubirya mkuu wa mkoa wa Njombe
Vile vile aliema âMaendeleo mnayoayaona katika nchi yetu yanaonekana kwasababu tuko katika mazingira ya amani,niwaombe wakati serikali tunapoendelea kushughulika na jambo hili niwaombe wananchi tuendelee kuonyesha ukomavu kuhimili jambo hiliâ aliongeza Marwa Rubirya
Amewathibitishia wananchi kuto kuachwa yeyote atakayebainika kuhusika na mauaji hayo âNiwathibitishie kuwa hakuna aliyehusika na uhalifu huu,ambaye hata chukuliwa sheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetuâ
Nao chama cha Mpainduzi CCM mkoa wa Njombe kupitia kwa mwenyekiti wake Jassel Mwamwala kimewataka vijana kuendelea kuwa watulivu kwa kuwa serikali inaendelea kulifanyia kazi swala hilo.
âNa ninny vija tunaomba tulieni acheni mihemko serikali yetu inafanya kazi na hakika tutapata jibuâalisema Mwamwala
Kijana huyo ameuawa kikatili wiki lililopita na watu wasiojulikana na mwili wake kutambuliwa baada ya siku sita ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mji wa Njombe kibena
Marehemu Emmanuel Mlelwa alihudumu kama mwenyekiti wa wanafunzi wa CCM wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Njombe kabla hajahamia mkoa wa Iringa ambako nako alikuwa akihudumu kwa cheo hicho akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumain kabla mauti hayajamkuta wakati akiwa likizo.
Recent Comments