Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania TANESCO Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera limezitaja sababu za kukatika kwa nishati hiyo kuwa ni pamoja na miti na migomba iliyo kwenye njia au jirani na njia kuu za Umeme
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja wa Shirika hilo Wilayani Ngara Bw.Isaack Mwijage ni kwamba ili kuzuia mkatiko wa Umeme mara kwa mara shirika hilo linaendesha zoezi la kusafisha njia
Bw.Mwjiage amesema kiutaratibu,njia kuu ya umeme inahitajika kuwa wazi muda wote kwa upana wa mita 10,na kutoa wito kwa wananchi kuepuka kupanda miti na migomba au kujenga nyumba chini ya njia kuu ya umeme kwa usalama wao na kwamba inasaidia wakati wa marekebisho ya miundombinu ya shirika hilo.
Kwa taarifa mbalimbali,Matangazo na huduma zetu za Simamia TV kanda ya ziwa wasiliana nasi kwa simu namba 0756432748
Recent Comments